Hospitali za umma nchini Kenya zimekuwa katika hali mbaya kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea./ Picha: TRT Afrika  

Serikali ya Kenya imesisitiza kuwa itawalipa madaktari shillingi za Kenya 70,000 (Dola 520) kwa mwezi, kama mshahara.

Madaktari hao wamekuwa kwenye mgomo kuanzia katikati ya mwezi Machi mwaka huu, baada ya kushindwa kufikia makubaliano na serikali kuhusu malipo ya madaktari wanafunzi.

Serikali ya Kenya inasema kuwa haiwezi kuendelea kuwalipa madaktari wanafunzi shilingi 206,000 (Dola1,530), wakisema ni jambo "lisilowezekana."

Baraza la Mawaziri la nchi hiyo, chini ya uenyekiti wa Rais William Ruto, lilisema katika taarifa yake ya Jumanne kuwa, kilio cha madktari hao kimepatiwa ufumbuzi, isipokuwa suala la mshahara wa madaktari wanafunzi.

Bima ya Afya

"Baraza la Mawaziri limepitisha maelekezo kuwa mishahara ya madaktari wanafunzi kuwa shilingi 70,000 (Dola 520)", huku likisema kuwa kwa sehemu nyingine, madaktari wanafunzi hulipwa 25,000 shillings (Dola190).

Madaktari wanaogoma pia wanaishinikiza serikali ya Kenya iwahudumie kikamilifu bima ya afya, kutuma wahudumu wa afya 1,200, makubaliano ya heshima ya kupandishwa vyeo, ​​na kuboresha mazingira yao ya kazi.

Baraza la mawaziri liliongeza katika taarifa yake kwamba lilikuwa limesuluhisha masuala ya "malimbikizo ya msingi ya mishahara, ufadhili wa masomo kwa masomo ya uzamili na bima ya matibabu."

TRT Afrika