Eneo la kaskazini mwa Kenya limekumbwa na mvua kubwa na maporomoko ya udongo katika siku za karibuni. Picha/ Reuters

Watu watano wamepoteza maisha na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka kaskazini mwa Kenya, maafisa na vyombo vya habari vya eneo hilo vimesema.

Miili ya wachimba migodi watano imeopolewa kutoka kwa mgodi wa Hillo, na watu wengine watatu hawajulikani waliko, kamishna wa eneo hilo Paul Rotich aliambia Reuters kwa njia ya simu Ijumaa jioni.

"Ripoti kutoka kwa waokoaji, polisi na wakuu wetu zinaonyesha wachimbaji wanane walikuwa ndani ya eneo la uchimbaji wakati kuta zilipoporomoka na kuwafukia wakiwa hai," Rotich alisema.

Wachimba migodi wawili waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini, shirika la utangazaji la NTV la Kenya liliripoti Jumamosi asubuhi.

"Eneo hilo liliporomoka kutokana na mvua," kamishna wa kaunti ya Marsabit David Saruni aliambia NTV.

Mamia ya watu wameuawa katika mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Kenya kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

TRT Afrika