Farida Tiemtore

Na Firmain Eric Mbadinga

Farida Tiemtoré, ni mwanasheria anayechipukia mwenye kupenda maendeleo ya wanawake nchini Burkina Faso, huku akiwa amedhamiria kuleta matokeo chanya katika jamii yake.

''Shauku yangu haiongozwa na kujitolea kwangu tu kitaaluma, lakini kila nyanja ya maisha yangu," anaiambia TRT Afrika.

Farida amekuwa akitoa uelewa miongoni mwa wanawake vijana, chini ya bendera ya Mashujaa wa Faso, kuhusu jinsi ya kuboresha hali zao za maisha.

Mapenzi yake katika utetezi yalianza akiwa Shule ya msingi , lakini alipata umaarufu mwaka 2019 alipoanzisha blogu, ambayo miaka miwili baadaye ilibadilishwa kuwa chama cha kutoa sauti kwa masuala ya wanawake.

‘’Kama Rais mwanzilishi wa chama cha wasichana, nimepata uzoefu muhimu katika utetezi, uhamasishaji wa jamii na usimamizi wa mradi.

"Kujitolea kwangu kitaaluma na kibinafsi kuna lengo moja la kusaidia kuunda Burkina Faso yenye haki na inayojumuisha zaidi kwa wote, ambapo haki za kimsingi za wanawake zinakuzwa," anasema.

Kupitia semina mbalimbali, Farida Tiemtore ameweza kuwajenge wanawake uelewa wa haki zao./Picha: TRT Afrika.

Wanachama wa chama cha Mashujaa wa Faso wameendesha mafunzo ya kuwaelimisha na kuwawezesha wanawake.

"Tunahakikisha kuwa wanawake wanapata haki sawa katika huduma muhimu na kuhakikisha kuwa wanapata taarifa sahihi,'' anasema Tiemtoré.

"Tunapambana na unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwasaidia waathirika kupitia sera zenye kuwalinda watoto wa kike na akina mama," anaelezea.

Kwa miongo kadhaa sasa, Burkina Faso imeghubikwa na uasi na kuifanya robo tatu ya nchi hiyo kuwa chini ya udhibiti ya vikundi vya kijeshi.

Ripoti ya hivi karibuni ya Oxfam, inaonesha kuwa zaidi ya wanawake milioni nchini humo wanakabiliwa na manyanyaso ya kijinsia, njaa na uhaba wa maji kutokana na machafuko ya siasa.

Oktoba 2023, Mashujaa wa Faso walianzisha "shule ya mashujaa", mradi unaolenga kutoa msaada wa elimu kwa watoto wenye wazazi walio vitani.

 Farida na kundi lake husaidia watoto wenye wazazi wanaoshiriki vita./Picha: TRT Afrika

"Tunataka kila mtoto aamke asubuhi akiwa na tabasamu la matumaini, akijua kwamba anapendwa, anaungwa mkono na kwamba wana mustakabali mzuri mbele yao," Tiemtoré aliwaambia waandishi wa habari wa eneo hilo wakati akikabidhi vifaa vya shule kwa walengwa.

Taasisi hiyo italipia watoto 15 ada zao za shule katika ada za shule kwa mwaka 2024/2025.

Katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake, chama kiliandaa kikao cha mafunzo kwa wanawake juu ya utengenezaji wa sabuni kama sehemu ya mpango wake wa ''usafi na mafunzo katika shughuli za kuzalisha kipato,'' anasema.

Mwaka 2019, blogu hiyo ilishinda tuzo ya Coup de cœur des internautes na zawadi ya mwanablogu bora wa jamii katika Tuzo nchini Burkina Faso.

Ili kufadhili shughuli zake, chama hicho hutegemea misaada kutoka kwa wafadhili na watu wenye mapenzi mema.

Chama hicho kinafurahia misaada hiyo katika kutekeleza shughuli zake mbalimbali.

TRT Afrika