anti france / Photo: AA

Awa Cheikh Faye

Mnamo Januari 28, maelfu ya watu walikusanyika Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, kusherehekea tangazo kuwa serikali ya Ufaransa ilikuwa inaondoa wanajeshi wake walioko katika taifa hilo la Kiafrika tangu 2018.

"Sherehe" hizo ziliambatana na uasi mkubwa wa umma nchini Ufaransa siku hiyo hiyo, wakati mamilioni ya raia wa Ufaransa walikusanyika kote nchini kupinga mipango ya mageuzi ya pensheni ya serikali ya Macron na shida inayoongezeka ya gharama ya maisha.

Kejeli hiyo haikuwashangaza watu nchini Burkina Faso

-Serikali ya Ufaransa inayozidi kutowasiliana na raia wake sasa inakabiliwa na miito ya kutaka kulegeza nguvu zake kwa makoloni ya zamani.

Sasa imeanza kufuata muundo flani. Wanajeshi wa Ufaransa waliondoka Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) mnamo 2021, miezi michache baada ya kumalizika kwa kutumwa kwa vikosi vyake vya jeshi nchini Mali.

Kuondoka katika nchi za Mali na Burkina Faso ni ishara zaidi katika ya mabadiliko ya uhusiano kati ya Paris na makoloni yake ya zamani, ambayo yanaonekana kudhamiria kufafanua upya "ushirikiano" ambao wengi wanaamini kuwa ni kubwa mno kwa Ufaransa.

Kushindwa kijeshi

Katika bara hilo, sera za Ufaransa zinazotajwa kuwa za ukoloni mamboleo zinapingwa kwa kauli mbiu na mabango kutoka kwa vijana, wanaokumbwa na umaskini na ukosefu wa ajira kwa miongo kadhaa.

Wanadai mfumo mpya zaidi wa ushirikiano na heshima kwa uhuru wa mataifa ya Afrika.

Hivi majuzi, hali hii ya kutopendezwa inaonekana kupamba moto, hasa kutokana na kuibuka kwa viongozi vijana nchini Mali, Guinea na Burkina Faso wenye mitazamo ya uzalendo ambao hawasiti kukataa hadharani mikataba na Ufaransa. Wanaamini kwamba mipango hiyo haitumiki kwa maslahi ya nchi zao.

Mchambuzi wa masuala ya usalama na jiografia Romual Ilboudo anaelezea mabadiliko ya mtazamo wa baadhi ya viongozi wa Afrika kuhusu Paris kama "sababu ya kizazi".

"Viongozi wa sasa wa Burkina, Mali, na Guinea hawajapitia ukoloni, wala kipindi cha uhuru, hivyo hawana utata. Ni kizazi ambacho kinadai kushughulikia kwa usawa na mkoloni wa zamani," Ilboudo aliiambia TRT Afrika.

"Kisha kuna mtazamo wa Ufaransa yenyewe. Paris haijabadilisha sera yake, na maoni yake juu ya makoloni yake ya zamani hayazingatii mageuzi ya kizazi. Kwa miaka mingi, mafadhaiko yameongezeka. Kukataliwa kwa jeshi la Ufaransa ni matokeo ya kufadhaika huku,” anaongeza.

"Kisha kuna mtazamo wa Ufaransa yenyewe. Paris haijabadilisha sera yake, na maoni yake juu ya makoloni yake ya zamani, hayazingatii kizazi kipya. Kwa miaka mingi, mafadhaiko yameongezeka. Kukataliwa kwa jeshi la Ufaransa ni matokeo ya kufadhaika,” anaongeza.

"Leo hii, uhusiano tulionao na Ufaransa ni ule uliowekwa na historia, si kwa uchaguzi wa kimkakati wa mataifa yetu," anasema Boubakar Bokoum, kiongozi wa Chama cha Afrika cha Ushirikiano na Utawala nchini Mali.

Operesheni za kijeshi za Ufaransa nchini Mali zilianza na Operesheni Serval ya 2013 dhidi ya waasi lakini hazikuweza kuzuia kuenea kwa vikundi vyenye silaha ambavyo vimeeneza ushawishi wao katika maeneo mapya zaidi.

Ndani ya muongo mmoja, magaidi wenye mafungamano na Daesh wameeneza ghasia zao huko Niger na Burkina Faso na hata kuathiri Ivory Coast na Benin.

Fedha za kikoloni

Suala lingine kuu ambalo huzua hasira katika eneo hilo ni la fedha.

Hili ni mada nyeti la Franc CFA, sarafu iliyorithiwa kutoka enzi ya ukoloni na inayotumika sasa katika nchi 14 za bara hilo.

Kwa miaka mingi, mjadala umekuwa ukiendelea barani Afrika kuhusu sarafu ya Kiafrika inayopaswa kuchukua nafasi ya Franc CFA.

Marc Bonogo, rais wa shirika la kiraia la Burkina Faso la Alliance of New Consciences, anasema kwamba "watu wengi wanaoongoza kampeni hii ni vijana chini ya miaka 30 wanaoishi na matokeo ya ukosefu wa ajira na umaskini unaoendelea. Mambo hayo yote yanahusishwa na Franc CFA.

"Uhuru wa kisiasa unaweza kuwepo, lakini kifedha na kiuchumi, nchi za Kiafrika zinazozungumza Kifaransa haziko huru," anaiambia TRT Akrika.

Hakika, wengi wanaona kuwa sarafu iliyorithiwa kutoka enzi ya ukoloni inazuia uwezo wa nchi za Kiafrika kudhibiti uchumi wao na kujiendeleza kwa uhuru.

Boubakar Bokoum, rais wa Chama cha Afrika cha Ushirikiano na Utawala nchini Mali, anasema kuwa "maslahi ya Ulaya daima yamekuwa yakiongozwa na ushindi na upanuzi.

"Upanuzi huo uliungwa mkono na masilahi ya kiuchumi. Kwa hivyo kilichosaidia kwa ufanisi kuundwa kwa Franc CFA - sarafu iliyovumbuliwa kwa roho ya sarafu ya Nazi - ilikuwa kuwezesha Ufaransa kufikia rasilimali inayohitaji Afrika."

Ilboudo anaelezea hili kama "kufungwa kwa sarafu yetu".

Franc CFA inazua swali la msingi la uhuru wa kiuchumi na kifedha kwa mataifa ya Afrika.

"Kama hatumiliki sarafu yetu, tunatapeliwa. Wasomi wa Kiafrika wameelewa thamani ya fedha na wameelewa jinsi CFA ya Kifaransa ilivyo na udanganyifu," anasema Boubakar Bokoum.

"Na kwamba uwekezaji mkubwa katika uchumi wetu leo ​​unaungwa mkono na IMF na Benki ya Dunia, ambayo ni ya udanganyifu, ubeberu wa Ulaya, na mtaji wa benki za kifedha duniani, yaani Marekani na Ufaransa," anaongeza.

Katika kutafuta Ushirikiano Upya

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mabadiliko thabiti kuelekea uhusiano wa karibu kati ya nchi za Afrika na mataifa mengine yenye nguvu kama vile Urusi, Uturuki na China.

Kwa wengine, hii ni matokeo ya mfululizo wa mambo, ikiwa ni pamoja na kutafuta fursa mpya za kiuchumi, tamaa ya kubadilisha mahusiano ya kimataifa na kuwa huru kutoka kwa utawala wa kifedha wa Magharibi na kuanzisha ushirikiano wenye usawa zaidi na mataifa kutoka mabara mengine.

Kwa wengine, kuibuka kwa hisia za kupinga nchi ya Ufaransa kwenye bara.

Marc Bonogo, hata hivyo, anasema, "hakuna chuki dhidi ya Ufaransa barani Afrika".

"Tunacholaani ni sera za Ufaransa barani Afrika. Watu wamegundua kuwa katika ushirikiano kati ya Ufaransa na mataifa ya Afrika, ni Ufaransa pekee ndiyo inafaidi huku Afrika ikitoka mikono mitupu, ndiyo maana vijana wa Kiafrika wameanza mchakato wa uwezeshaji wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.”

Romual Ilboudo anasema inasababishwa na hali ya juu ya ukarimu wa Afrika kwa ujumla na hasa Afrika Magharibi.

“Wafaransa wa Afrika Magharibi wameunganishwa vyema...Hata hivyo, lazima waonyeshe kujali wenyeji wao. Na maadamu kuna kuheshimiana, watakaribishwa kila wakati,” anasema.

Bokoum anasema Afrika leo inafahamu nguvu yake.

"Afrika inasema inatosha. Uporaji wa rasilimali unatosha. Udhibiti wa uchumi unatosha. Afrika inahitaji kujiendeleza," anasema.

"Hakuna sababu kwa nini tunapaswa kuwa na maliasili zote, pamoja na rasilimali zote za kiakili, na bado tuwe bara lenye maendeleo duni zaidi ulimwenguni."

TRT Afrika