Nchini Niger madarasa yenye vibanda yanayoshika moto ni janga la mara kwa mara. / Photo: AP

Na Guevanis Doh

Kutoweza kuwafikia watoto 21 wa shule waliokuwa wakipiga kelele walionasa kwenye tanuru la moto na moshi bila kutoroka bado unamlemea.

Zaidi ya miaka miwili baada ya mkasa huo wa kutisha, anachofikiri ni kelele isiyo ya kawaida ambayo bado inamfanya kuganda.

"Tulikuwa madarasani, ilikuwa saa kumi jioni, wanaume walikuwa wameenda kusali msikitini, watoto walikuwa wakifanya kazi zao za darasani chini ya uangalizi wa walimu. Ghafla tukasikia mayowe," Habiba anasema kuhusu moto huo siku hiyo katika Shule ya Pays Bays katika mji mkuu wa Niger Niamey.

Moto huo uliteketeza vibanda vya majani ya makazi ya shule hiyo kwa ndani ya dakika 10. Moshi ulikuwa mwingi sana hivi kwamba hakuna mtu aliyeweza kufika madarasani kujaribu kuokoa watu.

"Mwanaume mmoja alijaribu kuingia ndani na kuokoa watoto, lakini alizimia hata kabla ya kufika vyumbani," Habiba, Mkurugenzi wa Shule ya msingi, anaiambia TRT Afrika. "Moto umekuwa hadithi ya maisha yetu; hatusahau. Kinachoshangaza ni kwamba bado hatujui chanzo cha moto huu."

Uchunguzi ulioanzishwa na serikali bado haujatoa chochote kipya , angalau sio zaidi ya yale yaliyopatikana hapo awali ili kubaini chanzo cha moto wa hapo awali ulioteketeza shule zingine kote nchini.

Nchini Niger, madarasa yenye vibanda yanayoshika moto ni janga la mara kwa mara. Takriban watoto 50 wamepoteza maisha katika moto aina hiyo, katika kipindi cha miaka miwili pekee iliyopita. Kisa chahivi punde zaidi ni mnamo Februari 6 katika eneo la kusini la Zinder, karibu kilomita 1,000 kutoka mji mkuu Niamey.

Wanafunzi watatu walifariki kutokana na moto huo na kuibua upya mjadala wa ujenzi wa vyumba vya madarasa nchini.

Watoto wa shule nchini Niger wanakumbwa na hatari ya kusomea katika madarasa ya vibanda 

Mnamo Novemba 2021, wanafunzi 26 wenye umri wa kati ya miaka mitano na sita, walikufa katika moto ulioteketeza shule yao, iliyojengwa kwa mbao, mabati na majani, katika mkoa wa Maradi kusini mwa nchi.

Hii ilikuwa miezi saba tu baada ya maafa ya shule ya Pays Bas, ambapo wengi wa waathiriwa 21 walikuwa watoto wa chini ya miaka mitano.

Madarasa yanayowekwa katika vibanda vya majani, bila shaka, yameenea nchini Niger.

Yanajengwa kwa ajili ya ukosefu wa jumla wa miundombinu inayofaa, haswa katika shule kama Pays Bas, ambayo inahudumia wanafunzi 1,250.

Uzinduzi wa kampeni ya "Zero Straw-Hut Classrooms" mnamo Julai mwaka jana umekaribia kuanza kufanya mabadiliko lakini kidogo sana.

Walimu wanaongoza

Kulingana na UNICEF madarasa ya vibanda vya majani nchini Niger ni takribani 36,000. Idadi hiyo inaendelea kuongezeka huku zaidi ya wasichana na wavulana nusu milioni wanaanza elimu ya msingi kila mwaka, na kuongeza shinikizo kwenye miundombinu ambayo tayari haitoshelezi.

Kwa kuzingatia mazingira hayo, wajibu sasa ni kwa walimu kukaa katika tahadhari mara kwa mara kuhusu uwezekano wa kutokea kwa moto.

Habiba na wenzake katika shule ya Pays Bas wamefarijika kwamba taasisi yao sasa ina miundombinu bora, na salama zaidi.

“Msiba huo ulituumiza sana, tunamshukuru Mungu, hatuna tena vyumba vya madarasa vya majani, UNICEF imetuwezesha kujenga kiwanja kingine cha madarasa ambacho kwa sasa kinachukua watoto 439 wa shule ya sekondari,” anasema.

Serikali ya Niger bado haina mbinu mwafaka ya kujenga madarasa ambazo haziwezi kuathiriwa na moto

Baada ya maafa ya Aprili 2021, Habiba na wenzake walikatishwa tamaa kiasi kwamba walifikiria hata kujiuzulu na kuacha kufundisha.

"Washirika wetu walituunga mkono sana na kutushauri. Msaada wa kisaikolojia ulisaidia sana. Lakini hadi leo, kila kunapokuwa na kelele isiyo ya kawaida, tunapata wasiwasi na watoto wanaogopa. Tuko macho kila wakati haswa shule haina uzio, na hakuna ulinzi," anaeleza.

Rama Gouba, mzazi ambaye watoto wake watatu walinusurika kwenye moto wa mwaka wa 2021, ana ombi moja tu. "Serikali lazima iwalinde watoto wetu," anasema.

Elimu bila hatari

Kitengo cha serikali cha elimu imeanzisha hatua za kukomesha kuzuka kwa moto shuleni.

"Ili kumaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyofungwa, wizara ya elimu imetekeleza mkakati wa kujenga mifano mbadala ambayo ni ya kudumu, isiyo na gharama na inayokidhi viwango vya mazingira na elimu," anasema mkurugenzi Abdouramane Adama Brah.

"Kwa msaada wa serikali, tunatarajia kutimiza ahadi hii. Juhudi zinafanyika kuhakikisha upatikanaji wa elimu kwa wote."

Maofisa wa elimu wanaongea na walimu katika shule mmoja ambayo imejengewa madarasa mapya ambayo hayawezi kuathiriwa na moto | Photo UNICEF

Lakini kulingana na baadhi ya wahusika wa sekta ya elimu, serikali haina mbinu mwafaka.

Mahamadou Moussa, katibu mkuu wa Chama cha Mapambano dhidi ya Ajira ya Watoto nchini Niger (Alten), anaamini kwamba "serikali ya Niger na washirika wake wangeweza kufanya vyema zaidi".

"Ni lengo zuri kwa serikali kujaribu kufikia kiwango cha kutokuwa na madarasa ambayo si aina ya kibanda , lakini kinachokosekana ni mbinu ya utekelezaji. Itakuwa lini,leo kesho, miaka 5 au 10? Serikali iwe na nia ya dhati na itimize, ili wawekezaji wenye nia ya kusaidia wapate tayari kuna mfumo,” anaiambia TRT Afrika.

“Kama serikali inataka kujenga vyumba vya madarasa kwa nyenzo imara, tunahitaji kujua ingegharimu kiasi gani, kanda kwa kanda,” anaongeza.

Hadi suluhisho itapatikana kwa swala hili walimu, wazazi na washikadau wengine katika sekta ya elimu ya msingi nchini Niger wana chaguo moja tu: kuwa macho kwa ajili ya usalama wa watoto.