Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa  

Rais Marcelo Rebelo de Sousa amesema kuwa Ureno inawajibika na uhalifu ilioutenda wakati wa utumwa kipindi cha ukoloni, na kupendekeza kuwa kuna haja ya kulipa kutokana na uhalifu huo.

Kwa zaidi ya miongo minne, Waafrika milioni 12.5 walitekwa, na kulazimishwa kusafiri umbali mrefu na kupelekwa utumwani.

Wale walionusurika kwenye safari hizo waliishia kutumikishwa kwenye mashamba ya Amerika, hasa Brazili na Karibea, huku wengine wakinufaika kutokana na kazi zao.

Kukabiliana na uzamani

Ureno ilihusika na usafirishwaji wa zaidi ya Waafrika milioni 6, kuliko nchi yoyote katika Jumuiya ya Ulaya, lakini imeshindwa kukubaliana na ukweli.

Badala yake, enzi ya ukoloni wa Ureno, ambapo nchi zikiwemo Angola, Msumbiji, Brazili, Cape Verde na Timor Mashariki pamoja na sehemu za India zilitawaliwa na Ureno, mara nyingi huchukuliwa kuwa chanzo cha fahari.

Akizungumza katika hafla na waandishi wa habari wa kigeni siku ya Jumanne, Rebelo de Sousa alisema Ureno "inawajibika kikamilifu" kwa makosa ya siku za nyuma na kwamba uhalifu huo, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kikoloni, ulikuwa na "gharama".

"Tunapaswa kulipa gharama," alisema. "Je, kuna vitendo ambavyo havijaadhibiwa na waliohusika hawakukamatwa? Je, kuna bidhaa zilizoporwa na hazirudishwi? Ni vyema kushugulikia hili."

Kulipa fidia

Wazo la kulipa fidia au kufanya marekebisho mengine kwa utumwa linashika kasi duniani kote, ikiwa ni pamoja na jitihada za kuanzisha mahakama maalum kuhusu suala hilo.

Wanaharakati wamesema kuwa fidia na sera za umma za kupambana na ukosefu wa usawa uliosababishwa na siku za nyuma za Ureno, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa kimfumo, ni muhimu.

"Ni rahisi zaidi kuomba msamaha," aliongeza.

TRT Afrika