Zaidi ya raia 20 waliuawa katika shambulizi katikati mwa Mali, siku ya Jumamosi. /Picha: AA

Shambulizi lauwa zaidi ya raia 20 katikati mwa Mali, afisa wa eneo hilo alisema Jumapili.

Shambulio hilo la Jumamosi lililenga kijiji kimoja katika eneo la Bankass mjini Mopti, moja ya maeneo kadhaa kaskazini mwa Mali na katikati mwa Mali ambako makundi yenye silaha yamekuwa yakiendesha uasi tangu mwaka 2012.

Meya wa Bankass Moulaye Guindo, alisema washambuliaji wasiojulikana waliokuwa na silaha, waliwashambulia wanakijiji walipokuwa wakienda kufanya kazi katika mashamba yao.

"Jana tulihesabu vifo 19 lakini leo ni zaidi ya 20," alisema kupitia simu.

Wapiganaji walipata nguvu licha ya juhudi za kijeshi za kigeni kuwarudisha nyuma, na kuua maelfu na kuwafukuza mamilioni katika harakati hizo kwani wameshambulia miji, vijiji na vituo vya kijeshi.

Kushindwa kwa mamlaka kuwalinda raia, kumechangia mapinduzi mawili nchini Mali tangi 2020, moja katika nchi jirani ya Burkina Faso na moja nchini Niger.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT World