Tarehe Mei 29, 2024, Waafrika Kusini wataelekea kwenye uchaguzi. Chama kitachopata kura nyingi kitaunda serikali mpya. / Picha: AFP

Na

Sylvia Chebet

Kuwa na nafasi ya kuchagua katika demokrasia kunaweza kuonekana kama hali halisi, lakini kunaweza pia kusababisha kile wachumi wa kitabia wanaita "nafasi ya kuchagua iliyozidi ".

Wapiga kura milioni 17.6 wa Afrika Kusini wanaweza kukabiliwa na hali kama hiyo, wakati watakapoenda kwenye uchaguzi Mei 29, kuchagua serikali mpya ya kuendeleza mafanikio ya miongo mitatu ya baada ya ubaguzi wa rangi.

Tume ya Uchaguzi ya Afrika Kusini imesajili vyama 1,743 - idadi kubwa ya kushangaza inayoweza kuleta changamoto kusimamiwa. Mchakato huo ungekuwa mkubwa zaidi kama vyama vingine 800 havijafutiwa usajili na karibu vingine 100 vimekataliwa.

"Jukwaa limejaa," David Monyae, profesa mshiriki wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, anaiambia TRT Afrika.

Anasema kuwa vyama vilivyoundwa miongo kadhaa kabla ya mwisho wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994 vinagombania nafasi na vyama changa, vingine vikiwa na umri wa mwaka mmoja katika uwanja wa siasa.

Ingawa vyama vichache vipya vinaweza kung'oa mizizi, Monyae anafikiri kwamba vingi vyao vinaweza kutarajiwa "kufa mara tu baada ya uchaguzi".

Afrika Kusini imesajili vyama 1700, hata hivyo chama tawala na chama cha upinzani kuwa na ushawishi mkubwa. /Picha: AP

Kwa hivyo, wapiga kura wa Afrika Kusini wanawezaje kutenganisha ngano na makapi wanapotoka kupiga kura zao?

"Manifesto inafanana kwa kiwango fulani. Mtindo tu wa kufikisha ujumbe ni tofauti," anasema Monyae.

"Mada za kawaida zimetajwa: kufufua uchumi, kukabiliana na rushwa, kutatua masuala ya elimu na afya, usambazaji wa ardhi, na ruzuku ya ustawi wa jamii."

Huku mistari inayotofautisha vyama ikififia, wataalam wanaamini kuwa shindano hilo linatokana na umaarufu wa vyama.

"Kutafuta umaarufu umeanza," anasema Monyae. "Wana siasa wameanza kampeni zao na kutoa ahadi kwa watakayotekeleza."

Huku kukiwa na kampeni ya barabarani kabla ya uchaguzi, wapiga kura wamejikita kwenye vyama vitatu maarufu zaidi nchini Afrika Kusini.

Chama cha African National Congress

Chama cha ANC kimekuwa chama tawala nchini Afrika Kusini tangu 1994. Kilianzishwa mwaka 1912, ndicho chama kikongwe zaidi cha kisiasa katika taifa hilo.

"ANC imekuwa na fursa zake na kufikia hatua muhimu, lakini pia kuna mapungufu ambayo chama kinakubali, kama vile kutokuwa na uwezo wa kuhakikisha ugawaji wa ardhi sawa, msingi wa mapambano ya ukombozi," anaelezea Monyae.

Kutetea sera za kushughulikia ukosefu wa usawa, kutokomeza umaskini, na kukuza haki ya kijamii, ANC ilifurahia uungwaji mkono mkubwa karibu kila sehemu ya nchi kwa muda wake mwingi wa miaka 30.

Lakini katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kashfa za ufisadi zinazohusisha viongozi wakuu, mfumuko wa bei, na ukosefu wa ajira unaoongezeka umeondoa umaarufu wa chama tawala.

"ANC ilikuwa kiini cha vuguvugu la utaifa. Kwa vuguvugu lolote la utaifa, kama tunalitazama katika mtazamo wa kimataifa, maisha marefu katika mamlaka ni kati ya miaka 30 na 40," Monyae anaiambia TRT Afrika.

Kulingana na watafiti, ANC inaweza kupata chini ya 50% ya kura kwa mara ya kwanza katika miaka 30.

Monyae anaamini kwamba wakati muungano wa ANC na mapambano ya ukombozi ni wimbi kubwa ambalo linaweza kulisukuma au karibu na ufuo, ni lazima kuwe na mikakati ya kukabiliana na dhoruba.

Cyrill Ramaphosa wa chama tawla ameomba kubakia uongozini kwa muhula wa pili. Picha: Reuters

"Baadhi wanabishana kwamba hata kama ANC itapata 48% au 47%, upinzani unapaswa kuungana na kuwa pamoja. Lakini upinzani umegawanyika kama chama tawala," anasema.

Pia, matarajio ya serikali ya mseto yanawasumbua wananchi wengi.

“Kile kidogo tulichokiona cha serikali ya mseto katika ngazi ya serikali za mikoa na serikali za mitaa, kimekuwa balaa,” anasema Monyae.

Chama cha Democratic Allianca

Democratic Alliance (DA) ndicho chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini. Ilianzishwa mwaka 2000, inatetea demokrasia huria, utawala wa sheria, na uchumi unaoendeshwa na soko, ambayo yote yameisaidia kupata mvuto katika baadhi ya maeneo ya mijini.

"DA ni chama kilichotokana na cha zamani cha Demokrasia cha watu weupe," Monyae anabainisha. "Imeweza kushinda kile kinachojulikana kama jumuiya ya wenye rangi katika Mkoa wa Cape Magharibi lakini inajitahidi kupata kura ndani ya jumuiya ya watu weusi."

Chama cha Economic Freedom Fighters

EFF ni chama kilichotokana na chama cha ANC kilichoanzishwa mwaka 2013 na aliyekuwa Rais wa Umoja wa Vijana wa ANC Julius Malema.

Chama hicho kinatetea mabadiliko makubwa ya sera za kiuchumi za Afrika Kusini, ikiwa ni pamoja na kutaifisha viwanda na unyakuzi wa ardhi bila kulipwa fidia.

"Ingawa ni sehemu ya upinzani kiitikadi, haina tofauti na ANC," Monyae anasema. "Mtu angeiona zaidi kama kipengele cha itikadi kali cha ANC."

Kando na vijana, chama kimepata umaarufu haraka miongoni mwa wale waliokatishwa tamaa na mfumo wa jadi wa kisiasa.

"Kinaweza kuminyana na chama cha DA ," anasema Monyae.

Kundi la wapinzani

Vyama vingine mashuhuri katika mazingira ya kisiasa ya Afrika Kusini ni pamoja na Inkatha Freedom Party (IFP), Freedom Front Plus (FF+), United Democratic Movement (UDM), Pan Africanist Congress of Azania (PAC), African Christian Democratic Party (ACDP), na Chama cha Socialist Revolutionary Workers Party(SRWP).

Ingawa ni ndogo kuliko utatu ulioanzishwa, wachambuzi wanaamini kuwa vyama hivi vinachangia mjadala mzuri na tofauti wa kisiasa katika taifa la "rainbow".

Jacob Zuma heunda asishiriki katika uchaguzi wa Mei 29 kufuatia changamoto za kisheria. Picha: Reuters

Miongoni mwa vyama vipya , Arise South Africa, Rise Mzansi na Mkhonto WeSizwe (MK) wako mbali sana na kuthibitisha matokeo na ustahmilivo wao.

MK, kundi lililojitenga na chama tawala, lilimteua Rais wa zamani Jacob Zuma kama mgombea wake, lakini mahakama ya kikatiba ya Afrika Kusini iliamua Mei 20 kwamba Zuma mwenye umri wa miaka 82 hawezi kugombea uchaguzi wa Bunge kwa sababu ya kukutwa na hatia na kifungo jela kwa kudharau mahakama mwaka 2021.

Monyae anaamini kuwa uwepo wa Zuma katika kinyang'anyiro hicho ulikuwa wa kuudhi zaidi kwa ANC na Cyril Ramaphosa, bila kuwa changamoto kubwa katika mchakato wa kutafuta urais.

TRT Afrika