dddd

Huku sauti hasa za vijana zikipazwa kuhusu ukosefu wa ajira nchini Tanzania na katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki, wapo baadhi ya watu wenye ulemavu ambao licha ya hali ngumu ya kimaumbile lakini wameamua kupambana na kufanya kazi mbali mbali.

Miongoni mwa watu hao, ni Bahati John maarufu Bi. Khadija, mlemavu wa macho, lakini uwezo wake wa kuseka mikeka yenye rangi mbalimbali umeshangaza wengi.

ssddd

Bahati, mkazi wa Chamazi nje ya jiji la Dar es Salaam katika mahojiano yake na TRT Afrika, amesema kazi ya usuka wa mikeka amejifunza tangu mwaka 1994 kwa usaidizi wa marafiki zake ambao hawana ulemavu wa macho kama yeye.

Hii ilitokana na shauku yake ya kutaka kujifunza fani hiyo ya ususi wa mikeka. Na baada ya kumfahamisha rafiki yake, ndipo alipoamua kumfunza kwa kumuelekeza jinsi ya kushika ukindu.

“Rafiki yangu akaanza kunishikisha ukindu, kwa sababu wenye ulemavu wa macho, kazi zetu huzifanya kwa kugusa,” anasimulia.

Kutoka na hamasa aliyoipata ya kujifunza, Bahati alidiriki kutumia fedha alizopewa na mama yake kwa ajili ya kujikimu na kununua ukili ili aendelee kufanya mazoezi ya ususi.

dddd

“Kipindi hicho ukindu ulikuwa unauzwa shilingi 20,’’ anasema Bahati.

Kutokana na maelezo yake, kuandaa mkeka mmoja unaweza kuchukua hata mwezi mzima, hii inatoka na ukubwa wa mkeka huo.

Bahati anapatikana pembezoni mwa barabara katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, na wapiti njia ndio wateja wake wakuu.

Nahudumia familia yangu kwa kazi hii

Bahati ambae pia ni mama wa watoto wanne, wawili wakiwa bado ni wanafunzi, anajivunia kuhudumia familia yake kupitia kazi yake ya kusuka mikeka.

“Nikiuza mkeka wangu, natatua matatizo yanayowakabili watoto wangu,’’ anasema.

Mbali na wapita njia kumsaidia Bahati kifedha, lakini ameweka wazi kwamba, yeye sio ombaomba, na pembezoni hapo mwa barabara ni sehemu yake rasmi ya kazi.

TRT Afrika