Romania kumuondoa balozi wake nchini Kenya kwa matamshi yake ya ubaguzi

Romania kumuondoa balozi wake nchini Kenya kwa matamshi yake ya ubaguzi

Matamshi ya balozi huyo kuwaita waafrika Nyani yameshutumiwa vikali
Afisa mmoja wa Kenya anaelezea majaribio ya ubalozi wa Romania kuficha tukio hilo kama ‘fedheha’.  Photo: TRT Afrika

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, wizara ya mambo ya nje ya Romania imesema tayari imeanzisha utaratibu wa kumuondoa balozi wa Romania kutoka Kenya.

Wizara hiyo imesema maoni yoyote au maoni ya asili ya rangi hayakubaliki kabisa.

" Wizara ya Mambo ya nje ya Roma inajuta sana hali hiyo na inatoa pole kwa wale wote walioathiriwa," waziri wa mambo ya nje wa Romania amesema katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, " tunalaani vikali na kulaani tabia na mitazamo yote isiyoendana na kuheshimiana."

Wizara hiyo imeendela kusema kuwa " tabia na mitazamo kama hiyo haionyeshi kwa njia yoyote thamani ya kitaasisi na kibinadamu ambayo hatua ya kidiplomasia ya wizara ya kigeni ya Kiromania inasimamia."

Balozi wa Romania nchini Kenya Dragos Viorel Tigau anatuhumiwa kutumia matamshi ya kibaguzi wakati wa mkutano wa kundi la Ulaya mashariki ambapo aliwataja waafrika kama "nyani".

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Macharia Kamau alisema matamshi hayo "hayavumiliki na hayakubaliki katika umri wowote achilia mbali Karne ya 21 mjini Nairobi".

Katika ujumbe wake wa Twitter, Kamau alikashifu kile alichokitaja kama majaribio ya kuficha tukio hilo.

"Nimeshtushwa na kuchukizwa kusikia matamshi ya Balozi wa Rumania mjini Nairobi katika kuwarejelea wanachama wa Kundi la Afrika kama nyani wakati wa mkutano wa kundi la Ulaya Mashariki. Ni aibu kubwa kujaribu kuficha aibu hii. Hii haivumiliki na haikubaliki katika wakati wowote achilia mbali karne ya 21 jijini Nairobi," ameandika kupitia ukurasa wa twitter.

Balozi na ubalozi wa Romania hawajazungumzia shutuma hizo. Haijulikani ni wapi na lini tukio hilo lilitokea.

Tukio hilo linaungana na orodha ndefu ya mizozo ya kidiplomasia iliyochochewa na matamshi ya wanadiplomasia wa Magharibi yanayo chukuliwa kuwa ya kibaguzi dhidi ya Waafrika.

Mwezi Januari, ofisi ya mambo ya nje ya Ujerumani iliomba msamaha baada ya kutumia emoji ya chui kurejelea ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi barani Afrika.

Iliandika kwenye Twitter kwamba ziara ya Sergey Lavrov haikusudiwa kutafuta chui, bali kutumia safari hiyo kujaribu kuhalalisha vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

"@EbbaKalondo, hoja imeeleweka & samahani. Tunathamini washirika wetu wa Kiafrika. Tweet yetu haikuwa na maana yoyote ya kukera. Badala yake: 🐆 = mizinga ya Chui iliyotengenezwa na Ujerumani. Tulitaka kutangaza uwongo ambao Urusi inautumia kuhalalisha vita vyake vya uvamizi vya kibeberu dhidi ya Ukraine". iliandikwa na ukurasa wa mambo ya nje wa Ujerumani

Matamshi yanayodaiwa kuwa ya kibaguzi ya balozi wa Romania nchini Kenya yanasemekana kutolewa wakati wa mkutano wa kundi la Ulaya mashariki.

TRT Afrika