Google yatangaza Umoja, kebo mpya ya nyuzi za macho inayounganisha Afrika na Australia, na ushirikiano uliopanuliwa wa usalama wa mtandao na Kenya | Picha: Alphabet Google

Ikiwa na nanga, na kuishia au pengine kuanzia, nchini Kenya, njia ya kebo ya Umoja itapita Uganda, Rwanda, DRC, Zambia, Zimbabwe, na Afrika Kusini, kabla ya kuvuka Bahari ya Hindi kuelekea Australia.

"Miji mikubwa ya Afrika ikiwemo Nairobi, Kampala, Kigali, Lubumbashi, Lusaka, na Harare haitakuwa tena maeneo ya mbali yasiyofikika kutoka kwenye vituo vya kutua vya pwani vinavyounganisha Afrika na dunia"

Hayo yalikuwa maneno wakati wa tangazo kutoka Google ambapo Makamu wa Rais Brian Quigley alitangaza kebo mpya ya nyuzi za fiber itakayounganisha Afrika na Australia, na kupanua ushirikiano wa usalama wa mtandao na Kenya na kuendeleza ahadi yao ya mabadiliko ya kidijitali barani Afrika.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi, tarehe 23 Mei, Google ilitangaza kuboresha muunganisho na kuharakisha ukuaji wa kiuchumi kote Afrika kwa uwekezaji huu mpya na kusaidia kuongeza ukaribu na kutegemewa kwa muunganisho wa kidijitali kwa Afrika.

Umoja, neno la Kiswahili, linaungana na Equiano katika mpango wa Google wa African Connect.

Umoja utawezesha nchi za Afrika kuungana kwa uhakika zaidi na dunia nzima. Google walisema kuwa kuanza kwa njia mpya ya muunganisho tofauti na njia zilizopo ni muhimu kwa kudumisha mtandao thabiti kwa eneo ambalo kihistoria limekumbwa na kukatika kwa mtandao.

"Tunashukuru kwa ushirikiano kutoka kwa viongozi kote Afrika na Australia kuleta Africa Connect kwa watu, biashara, na serikali duniani kote." Quigley aliongeza.

TRT Afrika