Kifua kikuu

Coletta Wanjohi

Description: Mwaka huu Siku ya Kifua Kikuu Duniani imeadhimishwa kwenye mitandao ya kijamii kwa hashtag “#YesWeCanEndTB.

Shirika la afya duniani, WHO, linasema kifua kikuu ni mojawapo ya magonjwa hatari zaidi ya kuambukiza duniani, lakini tahadhari ndogo inatolewa kukabiliana nayo.

Kifua kikuu husambaa kwa njia ya hewa, wakati mtu aliyeambukizwa anakohoa, kupiga chafya au kutema mate.

"Chanjo pekee ya TB iliyotengenezwa hadi sasa, ni chanjo ya BCG, ina zaidi ya miaka 100, na haiwakingi vya kutosha vijana na watu wazima, ambao wanachangia zaidi maambukizi ya TB,” anasema Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

"Kila siku watu 4,100 wanakufa kwa TB na 25% ya hawa wanatoka Afrika," anasema Dkt Ahmed Ogwell, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika, Africa CDC.

Kifua kikuu kinaweza kuzuilika na kinatibika.

Kwa nini kesi za Kifua kikuu bado ziko juu barani Afrika?

Uchunguzi na upimaji wa TB haufanyiki ipasavyo

WHO inasema serikali za Afrika hazitoi takriban 22% ya ufadhili unaohitajika kukabiliana na TB

Janga la COVID-19 lilizingatia lilifanya magonjwa kama TB yasizingatiwe sana

Dawa mpya pia hazipewi kipaumbele

Ufadhili wa huduma za kinga, utambuzi na matibabu ya TB bado ni mdogo

Nchi nyingi nje ya Afrika pia pia kuimarisha tiba ya kuzuia TB bila mafanikio

TRT Afrika