Filamu za Kannywood huzingatia zaidi mapenzi na maisha ya familia na dansi na muziki | Picha: Falu Dorayi

Kumekuwa na mfananisho wa namna filamu katika lugha ya Kihausa na Bollywood, chimbuko mwanana la sinema kwa lugha ya Kihindi huko India ziliibuka. Bollywood inadhaniwa kushika nafasi ya pili baada ya Hollywood kutokana na mvuto wake kimataifa. Mfananisho huu kwa haraka-haraka unaonekana kama jambo lisilowezekana.

Ukweli ni kwamba Kannywood, jina ambalo tasnia changa ya filamu ya lugha ya Kihausa ilichagua kujitambulisha, ilibuniwa kwa kufananisha na Bollywood na mwandishi, Sunusi Shehu Burhan, katika toleo la Agosti 1999 la jarida la lugha ya Hausa Tauraruwa - lenyewe pia likijinasibu kwa kuiga jarida la Stardust la huko Bollywood.

Kama vile ambavyo tasnia ya filamu ya lugha ya Kihausa ilikuwa haifahamiki sana, na ubatizwaji wa jina hilo pia ulikuwa wa kwanza kwa tasnia ya filamu barani Afrika.

Neno Nollywood, kama kiwakilishi cha filamu za Nigeria, linatajwa kuwa lilibuniwa na Norimitsu Onishi wa gazeti la The New York Times mwaka wa 2002. Utambulishwaji huu umekuwa na mchango wa pekee katika uandaaji wa filamu nchini Nigeria, licha ya kuwa na vionjo vya aina mbalimbali vya kitamaduni nchini humo.

Huenda hili linaweza pia kuelezea mtazamo wa kile kinachoitwa “Sio-Nollywood” wa filamu zingine zinazotumia lugha asilia nchini humo.

Nollywood inatawaliwa na filamu za lugha ya Kiingereza (kama ambavyo Genevieve Nnaji, muongozaji wa Lionheart, kwa huzuni alivyong’amua wakati filamu hiyo ilipokosa uteuzi wa tuzo za Oscars mwaka 2019). Jambo hili liko hivyo tu kwa sababu ya Kiingereza hutumika kama lugha rasmi.

Hata hivyo, Nollywood haiwezi kusimama kama kitambulisho cha sinema cha taifa la Nigeria, hasa kwa vile Wanigeria wenyewe wamezoea kusema kwamba wanaundwa na "mataifa" tofauti.

Maudhui ya Kannywood

Jitihada za kuifanya ibakie tu kama sinema ya lugha asilia chini ya mwavuli wa Nollywood hazikufaulu. Sinema katika lugha zingine za Kinigeria hazijumuishi dhana ya ‘masimulizi ya baada ya ukoloni’ - ambayo ni moja wapo ya msukumo mkuu wa kinadharia wa sinema ya Nollywood, ambazo aghalabu huakisi nadharia ya mtunzi (k.m. Kunle Afolayan, Tunde Kelani, Izu Ojukwu).

Nje ya mkanganyiko huo, filamu za Kannywood zinatumia nadharia gani? Ni wazi kwamba nadharia kuu ya filamu zilizopo haziwezi kutumika katika filamu za Magharibi.

Ni kweli, tasnifu nyingi zilikuwa zimeandikwa juu ya uwakilishi wa wanawake katika filamu za Kihausa (zikirejea nadharia ya ufeministi), lakini hakuna hata moja iliyowasilishwa, ninayoijua, ambayo inazingatia vigezo vya uchambuzi wa kisaikolojia, Kimarxist, kijinsia au kiutunzi.

Uchambuzi mwingi katika sura za vitabu vilivyochapishwa, makala za majarida, mawasilisho ya kongamano na tasnifu zilijikita zaidi katika nadharia ya uchambuzi wa kifalsafa wenye kuchanganua mgawanyiko wa utamaduni na dini ya Wahausa katika filamu dhidi ya kile ninachokiita "mfumo wa hifadhidata wa kijamii".

Lakini sasa, ni nani anasema lazima tuwe na nadharia? Kama alivyosema Michael Chekhov, si tunaweza kusema mbinu ni nadharia?

Kimsingi vibwagizo vya masimulizi ya Kannywood vinajikitika katika miundo mitatu: hadithi za kimapenzi, migogoro ya familia, nyimbo na mtindo maridhawa wa uchezaji muziki. Hata hivyo, uimbaji na dansi umepungua sana kadiri miaka inavyosonga.

Kama watengenezaji filamu wengi wanavyosema, miundo hio ilikopwa kutoka Bollywood. Kiasi kwamba filamu nyingi za Kihausa ziliakisi moja kwa moja maudhui ya filamu za Bollywood.

Hivyo, inaweza kusemwa kuwa nadharia ya Kannywood, ni sehemu ndogo ya mafanikio ya kuvutia ya Bollywood.

Uzalishaji filamu wa Kannywood ulitofautiana na Bollywood tu katika lugha mpaka kufikia mwaka 2007, baada ya hapo ndipo mawazo mapya yakaanza kutumika katika lugha ya Kihausa.

Kwanza, Kannywood ikaanza kwa kubeba utamaduni halisi. Ikaondoka kuwa kibwagizo cha "wood". Hii ilitokana na kuanza kuakisi tamadaduni za maisha halisi ya kisasa mijini. Mafanikio makubwa ya tamthilia za Kihausa zilivyotakaa katika jukwaa la YouTube ni uthibitisho wa kutosha.

Nguvu kubwa inazidi kuwekwa katika uzalishaji wa tamthilia kuliko filamu za kawaida. Inaoekana katika tamthilia kunakuwa na uhuru wa ubunifu katika masimulizi.

Pili, Kannywood imekuwa kuinganishi cha kikabila - hadithi zinazogusia umuhimu wa jamii mbalimbali kuishi kwa umoja na mshikamano zimeandikwa.

Mfano ni Daɗin Kowa, manthari ya kufikirika katika mji mmoja kaskazini mwa Nigeria, ambayo imejuisha jamii tofauti zinaishi ndani ya chungu kimoja.

Tatu, utazamaji wake ni wa kimataifa - Kannywood inasambaa kwa kasi katika nchi zinazozungumza Kiingereza na Kifaransa barani Afrika, popote ambapo jamii ya Wahausa wengi wanaishi kama 'wenyeji', au wahamiaji.

Nne, neno Kannywood limetumika kwa zaidi ya miaka 24. Ni wakati sasa wa kuwekwa pembeni. Hata watumiaji wake wanaamini hivyo.

Hilo limethibitika kutokana na kuibuka kwa Kaddywood huko Kaduna kama mshindani wa Kannywood - sio kama utengenezaji wa filamu lakini kama vyama vinavyotetea umuhimu wa filamu, sura yake kwa jamii na maslahi makubwa kutoka kwa Serikali na wanasiasa. Hakuna aliyekuwa akizungumzia nadharia za filamu za uwakilishi.

Mwisho, na muhimu zaidi, Kannywood haifungamani tena na jiji la Kano - kama vile Hollywood na Bollywood (inayotokana na Bombay) - au hata Nigeria.

Ghana, Kameruni na Jamhuri ya Niger sasa zimegeuka kuwa vitovu vya utayarishaji, usambazaji na matumizi ya filamu za Kihausa bila ulazima wa kuzileta Kano kwa udhibiti au uuzaji.

Kwa hio zinajikuta ni filamu za Kihausa, si filamu za Kannywood. Kwa kuwa hakuna "utamaduni wa utayarishaji wa Kannywood". Haileti picha nzuri kuendelea kuzipa utambulisho filamu zinazotolewa kwa Kihausa kama filamu za Kannywood.

Hakika, hata watendaji katika tasnia ya filamu wenyewe na watazamaji wao wanawataja tu kama "Finafinan Hausa" (filamu za Kihausa). Kwa hivyo, sinema ya Kihausa ni lebo ya uhakika ya filamu za Kihausa, ndani ya muktadha wa kanuni mpya za uzalishaji.

Neno 'sinema au filamu' linaipa Kannywood nadharia ya kijumla. Nina hakika kuna vidokezo vingine vingi ambavyo mtu anaweza kuongeza kwa hizi. Kwa hivyo, ningependa kupendekeza "filamu ya Kihausa" kama njia mbadala ya "Kannywood"’.

Hii itakuwa sinema inayoakisi uasilia wa utamaduni ya watu wa Hausa, popote walipo.

(Mwandishi, Prof. Abdalla Uba Adamu, anafundisha katika Chuo Kikuu cha Bayero, Kano, Nigeria)

TRT Afrika