Masizi nyeusi ni matokeo ya mwako wa mafuta yasiyosafishwa / TRT Afrika

Na Charles Mgbolu

Wakiongozwa na wanaharakati wanne, wakaazi wa mji mkuu wa Rivers State, nchini Nigeria walifanya kampeni kwa miaka sita kulazimisha serikali kukandamiza mbinu haramu ya kusafisha mafuta inavyochafua jiji hilo kwa masizi meusi yenye sumu.

Port Harcourt hapo zamani ilikuwa 'Jiji la Bustani', mojawapo ya vituo vya miji vya Nigeria vilivyojaa kijani kibichi na bustani zilizopambwa kwa maua. Lakini hadithi yake ilibadilika kuwa nyeusi kwa mji huu mkuu wa eneo la Rivers lenye idadi ya zaidi ya watu milioni tatu.

Viwanda haramu vya kusafisha mafuta vinavyoendeshwa na watu wasio na ujuzi vinatoa moshi mwingi kwenye anga ya Port Harcourt.

Masizi nyeusi ni matokeo ya mwako wa mafuta yasiyosafishwa - yakining'inia hewani na kuunda safu nene kila mahali, kutoka kwa nyumba hadi kwa wanadamu. Watu walikabiliwa na kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa ya kupumua. Wengine hata walipatwa na saratani. Vifo vingi vilihusishwa na masizi meusi.

Ilichukua juhudi na uvumilivu na kundi la wakaazi - wakiongozwa na wanaume wanne – kuangazia mateso ya Port Harcourt. Ilichukua miaka sita kwa juhudi zao za kuonyesha matokeo.

Amah Onyedikachi, mwanaume mwenye miaka 38-year-old ni mmja wa walioongoza kampeni hii.

"Kila siku katika mtandawo wa tweeter tulitoa wito kwa wakazi wa Port Harcourt kukataa masizi,” Amah anaiambia TRT Afrika.

Hewa mbaya kila siku

Tatizo la Port Harcourt kusini mwa Nigeria lilikuwa suala la mjadala wa umma wakati masizi meusi yalipoonekana kwa mara ya kwanza mnamo 2016.

Ilikuwa ni kipindi ambapo usafishaji haramu ulienea katika eneo la Niger Delta, hasa katika mabwawa ya pwani ya Port Harcourt.

Ukosefu mkubwa wa ajira katika eneo la Niger Delta uliwavutia vijana wengi kwenye biashara yenye faida kubwa ambapo walichota mafuta ghafi kinyume cha sheria kutoka kwenye mabomba yanayomilikiwa na wafanyabiashara wakubwa wa mafuta na wanaomilikiwa na serikali.

Baadhi ya wasafishaji haramu hata walijenga mtandao wao wenyewe wa bomba uliozikwa chini ya ardhi ili kusafirisha uchafu uliowekwa kutoka kwa mabomba ya serikali.

Mafuta haya yasiyosafishwa hupitishwa chini ya joto jingi na kubadilishwa kuwa bidhaa tofauti - hasa mafuta ya taa na dizeli.

mamlaka nchini Nigeria imeimarisha juhudi za kutafuta na kuondoa mabomba haramu

Bidhaa iliyosafishwa inauzwa katika kwa soko isiyo halali nchini na hata kusafirishwa nje. Kulingana na ripoti ya shirika la 'Extractive Industries Transparency Initiative’, mwaka 2022, Nigeria ilipoteza mapipa milioni 619.7 ya mafuta yasiyosafishwa yenye thamani ya dola bilioni 46.16 kati ya 2009-2020.

Shirika la nchi zinazouza petroli yaonyesha kuwa nafasi ya Nigeria kati ya nchi zinazozalisha mafuta amabyo hayajasafishwa imerudi chini nyuma ya Angola na Libya, mwezi Septemba mwaka uliopita. Nigeria imelaumu hii kwa wizi mkubwa wa mafuta.

Kufikia Januari 2023, Nigeria imerejea kileleni, lakini ni baada ya mamlaka kuimarisha juhudi za kutafuta na kuondoa mabomba haramu. Amah anakumbuka mara ya kwanza alipoona masizi nyumbani kwake, mwaka wa 2016.

“Ilikuwa kana kwamba mtu fulani alikuwa amemwaga majivu kila mahali ndani ya nyumba yangu, Nakumbuka niliigusa na kujiuliza, ‘hii ni nini?’,” anasema.

Lakini hakuhitaji kutafuta majibu kwani mmoja wa marafiki zake wa karibu, Kingsley Adindu pia alikumbana na tatizo lilo hilo.

“Nilijua ni masizi mara tu nilipoigusa. Ilikuwa kama vumbi laini, lakini inatia doa popote inapoangukia ,” anakumbuka Adindu, 37, mwanamazingira na mmoja wa wanaharakati wanne.

Ilikuwa ni wasiwasi huu kuhusu mazingira na madhara kwa afya ya watu ambao ulisababisha kuanzishwa kwa kampeni yao mtandaoni.

Tunde Bello mwenye umri wa miaka arobaini na minane alijipata kama mwanaharakati wa mazingira alipounda ukurasa wa Facebook, na anwani ya Twitter aliziota “@StopTheSoot” ili kutoa ufahamu wa tatizo hilo.

Alianza kupokea picha zilizotumwa na wakaazi tofauti , zikionyesha masizi nyumbani mwao. Wengi walichukua picha za mikono na miguu yao zikiwa nyeusi.

Amah, Eugine Abels na Kingsley Adindu baadaye waliungana na kufanya kampeni ya umoja na yenye nguvu zaidi, na kusaidia kuendesha mijadala yenye makubwa sana kuhusu tatizo la masizi.

Eugine wa mwenye miaka 50 alizungumza sana katika mabaraza mengi ya mazingira, ndani na nje ya mtandao, kuhusu athari ya muda mrefu ya masizi ya kwa afya na ikolojia .

Kingsley alijulikana kwa kutoa kila mara vidokezo vya afya na usalama mtandaoni kuhusu jinsi ya kukabiliana na masizi.

Pamoja walifanya maandamano ya amani mnamo 2018 pamoja na mamia ya wakaazi wa Port Harcourt.

Baada ya mwezi mmoja wa kampeni, shinikizo la umma lilipoongezeka kwa mamlaka kuchukua hatua, serikali ya Jimbo la Rivers ilianzisha kikosi kazi kushughulikia suala hilo. Kikundi hicho kilitambua rasmi chembe hiyo isiyoeleweka kuwa masizi meusi.

Hata hivyo, hawakuwa wamefaulu kufanya hatua madhubuti dhidi ya usafishaji haramu wa mafuta.

Muuaji kimya

"Masizi meusi ni matokeo ya mwako usio kamili," anasema Dkt. Selegha Abrakasa, mkufunzi katika Chuo kikuu cha Port Harcourt.

"Kwa sababu wasafishaji haramu hutumia vifaa ambavyo havifai katika mchakato wa kusafisha mafuta, taka nyingi za mabaki hutokea na kuingia kwenye anga kwa njia ya masizi meusi," Abrakasa anaiambia TRT Afrika.

Masizi ni mojawapo ya aina mbaya zaidi za uchafuzi wa hewa.

Timu ya madaktari wa watoto katika idara ya madakitari wa watoto, katika hospitali ya fufundishia ya Chuo Kikuu cha Port Harcourt, ikiongozwa na Dk Agnes Fienemika, ilichunguza kuenea kwa magonjwa ya kupumua kati ya watoto chini ya miaka mitano huko Port Harcourt kwa miaka miwili.

Walitumia kesi zilizoripotiwa katika hospitali ya watoto kama sampuli ya majaribio na wakapata ongezeko la visa vya kushidwa kupumua vizuri miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano kati ya Septemba na Desemba 2016.

Timu ya dkt. Fienemika iligundua kuwa kipindi cha 2016 kiliambatana na kuonekana kwa masizi meusi huko Port Harcourt. Matokeo yao yalichapishwa katika jarida la tiba ya kupumua mnamo 2018.

Profesa Best Ordinioha, mtaalamu wa afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Port Harcourt, anaiambia TRT Afrika kwamba masizi yanaweza kusababisha athari mbaya za mzio.

" Athari za haraka za kupumua kwenye masizi ni pamoja na shambulio la pumu, haswa kwa wagonjwa wa pumu na watu walio na shida ya moyo na mapafu."

Waokoe watoto

Amah anasema kwamba katika siku za mwanzo za kampeni yao, walilenga watoto.

"Tulianza kuweka mitandaoni mashauri kwa mashule kuhusu jinsi ya kuwalinda watoto. Kulikuwa na ushirikiano mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na, cha kushangaza, ukosoaji pia. Baadhi ya watu walitushtumu na kudai tulikuwa hatusemi ukweli ,” Amah anasema.

Kingsley Adindu alipata athari za masizi kwa watoto moja kwa moja.

" Nilitumia pesa nyingi kununua dawa na kulipa ada za hospitali. Ilikuwa ya kukatisha tamaa,” Adindu anaiambia TRT Afrika.

Adindu anasema afya ya watoto wake sasa imeboreka.

"Nilikuwa nikipeleka watoto wangu (mvulana, wakati huo akiwa na umri wa miaka 4, na msichana wa mwaka mmoja) hospitalini angalau mara moja kila wiki kutokana na magonjwa ya kupumua. Lakini hatujakuwa na sababu ya kwenda tangu kuanza mwaka huu.”

Eugene anasema alipigwa na butwaa aliposoma kuwa vipengele vya chuma vyenye sumu hupatikana kwenye masisi.

"Niligundua kuwa ina vitu vinavyosababisha saratani na zebaki. Niliingiwa na hofu kwa sababu ya hali duni ya huduma zetu za afya. Hii ilikuwa hukumu ya kifo kwa watu,” Eugine anaongeza.

Mwaka 2022, serikali ya jimbo tena ilianza kuvamia maeneo haramu ya kusafisha mafuta.

Takriban watu 16 waliohusika katika biashara hiyo haramu walikamatwa, na wengine 19 wakatangazwa kuwa wanasakwa.

Zaidi ya viwanda vidogo 100 ya kusafisha mafuta haramu ziliharibiwa katika maeneo tofauti kote jimboni. Uvamizi mwingi ulitokea katika eneo la serikali ya Mtaa unaitwa Khana, ambapo angalau maeneo 20 ya kusafisha mafuta haramu yaliharibiwa.

"Baadhi ya wachimbaji hawa haramu wa mafuta walikuwa na silaha nzito na walitufyatulia risasi wakati vikosi vya usalama vilipokaribia eneo lao kabla ya kutorokea kwenye vinamasi," Bariere Thomas, mwenyekiti wa halmashauri ya eneo la serikali ya mtaa wa Khana, anaiambia TRT Afrika.

"Nimeona tofauti kubwa kuhusu masizi kwenye madirisha yangu. Sioni tena chembe chembe alfajiri kama nilivyokuwa nikifanya kila siku”.

Vita havijakwisha

Lakini mwanaharakati Abrakasa anaonya kuwa changamoto haijakwisha.

“Serikali lazima ihakikishe wachimbaji haramu wa mafuta hawaruhusiwi kuibuka tena. Ikiwa wangefanya hivyo, basi kila kitu kingekuwa sawa."

"Bado kuna baadhi ya viwanda vidogo vidogo visizo halali za kusafisha mafuta vinazofanya kazi katika maeneo ya mbali bila kusumbuliwa, kwa hiyo hii inahitaji kuchunguzwa".