Nchini Ethiopia wanawake wanashiriki kwa kina katika kampeni ya upandaji miti/ AA

Katika siku moja tulivu ya mwezi wa saba mwaka 2019, Ethiopia ilipanda jumla ya miche milioni 350 katika tukio lililovunja rekodi katika kuonesha kujitoa na uvumilivu.

Sababu iliyo nyuma ya hili tukio la upandaji miche kwa wingi ni la hasara na maumivu. Kwa mujibu wa makadirio ya Umoja wa Mataifa, Misitu imepungua nchini Ethiopia kwa asilimia 4 katika miaka ya 2000, chini kutoka asilimia 35 kwa karne iliyopita.

Idadi hii ni ishara za wazi kabisa za changamoto ya mabadiliko ya kimazingira kama ukame na ongezeko la joto ililiamsha taifa kuchukua hatua stahiki.

Mataifa mengine ya Afrika yaliiga mfano wa Ethiopia kwa kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la watu na utaratibu wa usimamizi wa ardhi usio endelevu.

Ethiopia pia inalenga kuingiza uelewa wa mazingira katika kizazi kipya. Picha: AFP

Itakuwa ni vita ya muda mrefu kwa bara la pili kwa wingi wa watu duniani.

Miti kwa uokoaji

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu shughuli za kibinadamu inasema kwamba Afrika ya Mashariki, ukanda wa pembe ya Afrika pia ukijumuishwa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu amesema eneo panakabiliwa na ukame wa muda mrefu , Ikiwa ni pamoja na misimu 5 ya mvua chini ya kiwango inayotarajiwa kutishia usalama wa chakula.

Kwa baadhi ya sehemu za Kenya, Somalia na Ethiopia, kipindi cha ukavu au ukame ni kirefu na kikali zaidi katika historia ya hivi karibuni na kimeathiri zaidi ya watu milioni 36, inaendelea kueleza.

Mwezi wa kumi na moja mwaka jana, mashirika ya kibinadamu yalionya kuwa kutakuwa na upungufu wa mvua chini ya kiwango tarajiwa na hali hiyo inaweza kuendelea mpaka msimu wa mwezi Machi na mwezi Mei kwa mwaka 2023. Kipindi hiki cha ukavu kimepewa jina la “”Janga la kibinadamu”.

Katika mchanganuo wake wa Januari 2023, Mamlaka ya Usimamizi wa Ukame wa Kitaifa umeelezea kwamba mwaka jana mwishoni, kwenye mwezi wa Oktoba mpaka Disemba kipindi cha mvua fupi kilikuwa ni dhaifu. Ikichagizwa na misimu minne ambayo mvua haikunyesha kabisa, hali ya ukame kwa baadhi ya maeneo imebaki kuwa ni mbaya zaidi.

Mamlaka inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 4.4 wanaweza kuhitaji msaada kwa mwaka 2023.

Wakati dalili za awali za mabadiliko ya tabianchi zilipoanza kujionesha, mwaka jana Kenya iliingiz katika zoezi la upandaji wa miti kwa wingiili kukabilianna na uharibifu wa ikolojia.

Mwezi wa kumi na mbili, Rais William Ruto alizindua kampeni ya upandaji miti kitaifa na uhifadhi ardhi ikilenga kupanda miti ipatayo bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Ukame huo umesababisha uhaba wa chakula unaoathiri mamilioni ya watu na wanyama. Picha: AA

“Kama kila mmoja wetu atashiriki kwa nafasi yake, ni sawa na miti 300 kwa kila Mkenya,” Katibu wa baraza la mazingira na misitu alisema wakati wa uzinduzi.

Ethiopia bado inaendelea na njia ile iliyoichagua mwaka 2019.

“Miaka minne katika zoezi la utekelezaji wa Mpango wa Urithi wa Kijani, tumefanikiwa kukusanya wa Ethiopia milioni 25 katika nchi nzima kupanda mbegu bilioni 25 ambayo ni sawa na mbegu 250 kwa kila mwananchi,” waziri mkuu Abiy Ahmed alisema katika mkutano wa COP27 uliofanyika nchini Misri mwaka jana.

Kukuza asili

Ofisi ya baraza la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira (UNEP) inasema kwamba kurudisha ikolojia ambayo imeharibiwa inaweza kuleta matokeo mazuri ndani ya kipindi cha muda mrefu.

Levis Kavagi, Mratibu wa Mpango wa Ikolojia na Biodiversity katika ofisi za UNEPkwa Afrika,ameiambia TRT Afrika kwamba upandaji miti na urudishaji wa misitu ni hatua muhimu ya kupata hewa ya ukaa na kuirudisha na kuihifadhi katika ulinzi wa mimea.

“Ufanisi wa upandaji miti upya na ukuzaji wa misitu utategemea na kiwango kitakachofikiwa. Eneo kubwa ni bora zaidi.Sehemu za miti zilizotengwa zina uwezo mdogo wa kutoa udhibiti unaohitajika wa hali ya hewa kubwa na ndogo ya eneo. Kwa kiwango kinachofaa misitu huchangia katika udhibiti wa hali ya hewa, na kwa mzunguko wa kihaidrolojia wa eneo hilo,” anaeleza Kavagi.

Anaongeza kwamba miti ina uwezekano wa kustawi kwenye maeneo ambayo ilikuwepo tangu mwanzo.

Rais wa Kenya Ruto alizindua kampeni ya upandaji miti mwaka wa 2022 ili kuokoa mazingira. Picha: KFS /Tovuti

“Kwa sababu hii, ni muhimu kupanda miti katika maeneo yake ya asili ambako kuna uwezekano mdogo sana wa kukaribisha maotea au aina vamizi. Pili, aina za asili huzoea mazingira na udongo husaidia kwa kiasi kikubwa viumbe hai tofauti na aina za kigeni. Miti ikishapandwa, miti ya asili itazaliana kiasili.”

Muhammed Lamin SaidyKhan wa Climate Action Network (CAN) anasema kwamba kwenye maeneo ambayo yameathiriwa na ukame, upandaji miti lazima ufanyike mara kwa mara. Climate Action Network ni mtandao wa ulimwengu wa asasi za kiraia zinazopambana na mabadilito ya tabianchi.

“Kuna miti ambayo ina uwezo wa kustahimili ukame ambayo unaweza kuanza nayo haasa kwenye maeneo yenye ukame. Halafu sasa, pale unapofanikiwa kugeuza mazingira kuwa ni ya kijani , mazingira yale yataruhusu aina zote za miti kupandwa.”

Serikali ya Ethiopia ilikuwa imetoa miche kwa wananchi kupanda. Picha: AFP

Lamin anaendelea kusisitiza kwamba, ili mpango wa upandaji miti wa kitaifa uwe endelevu, serikali ni lazima itenge bajeti kwao na kuhamasisha moja kwa moja ushiriki wa wananchi.

Hata hivyo, UNEP, inaonya kwamba makossa kadhaa yameshafanyika katika zoezi la upandaji miti na urejeshaji wa misitu.

“Kwa mfano, kutumia nnjia na aina za miti zisizofaa, katika maeneo yasiyostahili, na bila ushirikishwaji kati ya watendaji, wanasayansi, na wananchi wa kawaida, matokeo yake watu na mazingira wameathiriwa na uvamizi wa aina ngeni katika baadhi ya maeneo,” Anafafanua Kavagi kutoka UNEP.

“Mifumo yote ya ikolojia kutoka maeneo yenye ardhi yenye ukavu hadi maeneo yenye ardhi yenye unyevu, toka kwenye vilele vya milima mpaka katika vilindi vya bahari – zinatoa nafasi ya kuthaminika na kuhifadhi bioanuwai za kipekee. Kupanda miti katika maeneo yenye nyasi za asili kunaweza kuharibu zaidi kuliko kuponya.”

TRT Afrika