Disturbed person / Photo: Getty Images

Kila mtu ana nafasi yake tunapozungumzia kuhusu kujiua: watu binafsi, wanafamilia, marafiki, wafanyakazi wenzako, wanajamii, viongozi wa dini pamoja na wanasiasa. Visa vya kujiuwa vinatokea kila siku, na masuala hayo sharti yapatiwe ufumbuzi wa kila siku.

Hatua muhimu ni kwamba ‘inaanzia na wewe.’ Watu sharti wabaini kwanza kwamba wanahitaji msaada na wachukue hatua stahiki.

Siku ya Kuzuia Kujiuwa ni siku moja tu ambayo elimu inatakiwa kutolewa kwa wingi kuhusu masuala ya kujiua, iwe ni majaribio au hatua zenyewe.

Katika maadhimisho yaliyofanyika mwaka huu, Shirika la Afya Duniani WHO imesaidia kutoa nyenzo za kuzuia watu kujiua, hatua ambayo inaongeza jitihada za watu wanaokabiliwa na changamoto hiyo ya kukata tamaa.

Mbinu mpya zilizobuniwa kuepusha watu kujiua ni muhimu kwa nchi za Afrika ambapo kiwango cha visa vya kujiua ni kikubwa kuliko kiwango cha dunia cha visa tisa kwa watu laki moja kwa mwaka.

Baadhi ya nchi zimepiga marufuku kujiua au hata kujaribu kujiua. Hii inafanya mapambano dhidi ya visa vya mauaji kuzidi kuwa magumu na kulifanya bara kuwa mbali na kufikia malengo endelevu ya umoja mataifa ya kupunguza visa vya mauaji kwa kiwango cha thuluthi moja kufikia mwaka 2030.

Miongoni mwa nchi hizo ni Eswatini, nchi ya kifalme kusini mwa Afrika, ambayo idadi yake ya watu milioni 1.2 inakabiliwa na tishio la watu kujiua kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo afya ya akili, mfumo wa maisha, tatizo la ajira na mahusiano.

Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Wagonjwa wa Akili ya Eswatini. Picha TRT Afrika

Vijana

Nchi hii iko katika orodha ya nchi kumi zenye idadi kubwa ya visa vya kujiua. Katika ripoti yake, Benki ya Dunia, inasema kwamba Eswatini ni ya pili baada ya Lesotho katika bara. Nchi mbili hizo, zina asilimia 72.4 na 29.4 ya idadi ya watu kujiua.

Swali la msingi

Eswatini ni moja ya nchi ambazo zinakuwa nyuma katika kukabiliana na tatizo la afya ya akili katika kufuata sheria.

Huku katika nchi nyingi, kujiua kunaangaliwa kama sehemu ya tatizo la akili, Eswatini waathirika wa kujiua wanaangaliwa kama wahalifu kuliko watu wanaohitaji msaada.

Wanafunzi wengi mara nyingi hushindwa kuomba msaada wanapokabiliwa na hali ngumu ya kifedha wakiwa chuoni. Badala yake wanaamua kujitoa uhai.

Mnamo mwaka 2022, takriban arobaini katia ya wanafunzi wa chuo waliopo katika miji mikubwa ya Eswatini walijaribu kujiua kwa sababu ya kushindwa kulipa ada.

Hivi karibuni, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Swatini Action Against Abuse, SWAGAA, Nonhlanhla Dlamini, mitandao ya kijamii imechangia vijana kuwa na matarajio makubwa maishani. Kutokana na ushawishi wake, imesababisha vijana wengi kutumia kama kipimo cha mafanikio ya maisha.

Unyanyasaji wa kijinsia pia unaonekana kama sababu kubwa inayofanya watu hasa wanawake kujiua hasa wale ambao hawawezi kutoa taarifa kwa kuhofia unyanyapaa.

Gari linalotumika kubeba wagonjwa wa afya ya akili wasio na vurugu limejaa nje ya Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa ya Wagonjwa wa Akili. Picha: TRT Afrika

Utafiti uliofanywa mwaka 2022 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana unaonyesha kuwa ni mara chache mno hatua huchukuliwa pindi visa vya unyanyasaji vinapotokea.

Jukumu la vyombo vya habari

Nchi hii na bara lote kwa ujumla linaweza kutumia mbinu hizi kukabiliana na changamoto hiyo, moja wapo ikiwa ni Kanuni ya kujitoa uhai ya 1959, sehemu ya 4 kwa Eswatini, ambayo inataja kujiua kama uhalifu.

Vyombo vya habari, na uwezo wake wa kuwajibisha, kuelimisha, kuhabarisha na kupitisha taarifa, sharti ibebe jukumu la kuwahamasisha watu watoe taarifa pindi wanapokuwa na matatizo, kupata mtu wa kuzungumza nae, na kupata wana familia watakaochukulia vitisho vya kujiua kwa umuhimu wake.

Bonisile Makhubu, mwandishi wa habari Eswatini

Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi si lazima yaakisi maoni, maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT Afrika