Nyota wa Uingereza Jude Bellingham aliisaidia Real Madrid kuifunga Osasuna 4-0 mechi ya jumamosi ya la Liga. / Picha: AFP

Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 20, ambaye alijiunga na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani mwezi Julai, tayari amefunga mabao 10 katika mechi 10 kwenye mashindano yote ya miamba hao wa uhispania.

Nyota huyo wa soka wa Uingereza Jude Bellingham alifunga mabao mawili Jumamosi katika mechi ya La Liga ya uhispania katika dakika ya 9:54 walipocheza nyumbani katika Uwanja wa Santiago Bernabeu na kusaidia Real Madrid kuizaba Osasuna 4-0.

Hata kabla ya mechi hiyo dhidi ya Osasuna, kiungo huyo tayari alikuwa amefunga mabao sita katika mechi saba, pamoja na kuweka pasi mbili ndani ya La Liga.

"Mimi pia amenishangaza kwa sababu ingawa ana umri wa miaka 20, lakini anaonekana kama ana miaka 30 kwa sababu ya tabia na mtazamo wake," alisema kocha wa Madrid Carlo Ancelotti.

Kiungo huyo amekuwa mchezaji muhimu wa Madrid tangu alipojiunga nao kwani pia mapema wiki hii, alifunga na pia kumuandalia pasi la bao Vinicius Junior katika ushindi wa Madrid wa 3-2 dhidi ya Napoli kwenye mechi ya ugenini katika Uwanja wa Diego Armando Maradona, nchini Italia.

"Hakukuwa na njia bora zaidi kwa Jude kumheshimu nyota marehemu wa Argentina," liliandika gazeti la Marca la uhispania.

"Ingawa halikuwa goli la Maradona dhidi ya England, lakini kwa hali yoyote, nambari 10 huyo wa kihistoria angekuwa na fahari kuifunga."

Madrid inaonekana kupiga bonge la dili kwa kulipa euro milioni 103 (dola 108 milioni) Kwa Dortmund kumtia kapuni kiungo huyo wa zamani wa Birmingham City na kwa kweli inaonekana kuwa wamepata thamani ya pesa walizotoa.

Hata ingawa Madrid walikuwa sana wanamwinda staa wa Paris Saint-Germain na mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe, Bellingham anaonekana kuwa msajiliwa wao bora zaidi.

Jude Bellingham baada ya Mechi 9 amefunga mabao 8 na kutoa pasi 3.

Zinedine Zidane baada ya Mechi zake 9 za kwanza Real Madrid, ndani ya msimu wa 2001-02, alikuwa amefunga mabao 4 na kutoa pasi lililopelekea bao.

Cristiano Ronaldo baada ya Mechi zake 9 za kwanza Real Madrid ndani ya msimu wa (2009-10) alikuwa amefunga mabao 9 na kutoa pasi moja lililopelekea bao.

TRT Afrika