Na Lulu Sanga
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia ofisi ya rais Ikulu nchini Tanzania amewakaribisha wachezaji na timu ya Yanga mashabiki na wadau mbalimbali ili kupongeza mafanikio ya timu hiyo.

Hafla hiyo ya kuwapongeza Yanga imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo rais Samia alitumia fursa hiyo kuwapongeza na kuhamasisha ushiriki hai katika soka la Tanzania.

Yanga ilipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika michuano ya fainali ya Mashindano ya Shirikisho Afrika (CAF)

Miongoni mwa wageni waliohudhuria ni viongozi mbali mbali wa kisiasa na wadau wa soka nchini Tanzania.

Watu maarufu pia walialikwa kushuhudia mapokezi hayo ya heshima kwa timu ya yanga ilioitoa Tanzania kimasomaso baada ya kuisukuma mpaka katika kilele cha fainali za CAF

Mashabiki pia hawakuachwa nyuma kwani baadhi ya watu mashuhuri wengi waliohudhuria shughuli hiyo baadhi yao ni mashabiki kindakindaki wa timu ya yanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pia alipokea Medali kama ishara ya shukrani kutoka kwa Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said wakati wa hafla ya kuipongeza timu ya Yanga

Baada ya mazungumzo na pongezi Rais Samia pia alishiriki chakula cha usiku na wageni wote waliokua wamealikwa katika hafla hiyo.


Tanzania inapata fursa hii ya kutinga katika fainali za CAF miaka 30 baadae na kufanya ushindi wa yanga kutinga fainali kuirejesha nchi hiyo ya afrika mashariki kwenye ramani ya soka Afrika.
