TP Mazembe kutoka DRC, imetoka sare ya 0-0 dhidi ya Mabingwa watetezi wa kombe hilo kutoka Misri, Al Ahly SC/Picha : TP Mazembe 

Washindi mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imetoka sare ya 0-0 dhidi ya Mabingwa watetezi wa kombe hilo kutoka Misri, Al Ahly SC kwenye mchuano wa mkondo wa kwanza wa Nusu Fainali uliooandaliwa Mjini Lubumbashi, DRC, Jumamosi.

Timu hizo zitakutana tena katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Ijumaa, tarehe 26 Aprili 2024 kwa mechi ya marudio.

Ingawa Mazembe imesikitishwa na kutotikisa wavu nyumbani, macho yote sasa ni kwa Cairo kwani pande zote bado zina matumaini ya kufika fainali.

TP Mazembe inalenga kufika fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 tangu waliopofuzu fainali za Ligi ya Mabingwa ya Totalenergies CAF 2015.

Al Ahly (Misri), Tp Mazembe (DR Congo), Espérance Sportive Tunis (Tunisia) na Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) ndizo timu nne zilizosalia kuwania taji hilo maarufu la soka barani Afrika.

Klabu hizo nne, zilizosalia nusu fainali, zimewahi kutwaa jumla ya mataji 21 ya Ligi ya Mabingwa ya CAF kati yao.

Mabingwa Watetezi Al Ahly ndio wanatawala kwa mataji kumi na moja, Mazembe wanafuata na matano, ES Tunis na manne, Na Mamelodi Sundowns na taji moja.

TRT Afrika na mashirika ya habari