Messi, ambaye atafikisha umri wa miaka 36 mnamo Juni 24, anakuwa mchezaji huru rasmi mkataba wake na Paris Saint-Germain ya Ufaransa utakapomalizika / Picha: Reuters

Mwanasoka machachari wa kimataifa Lionel Messi huenda akaingia katika dimba la soka huko Marekani.

Messi anahusishwa na timu ya soka ya inter Miami CF ya marekani, vyombo vya habari vya kimataifa vinaripoti.

Endapo nyota huyo wa michuano ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Argentina atatia saini mkataba wa kujiunga na MLS ya marekani basi atakuwa ametia teke kurejea Barcelona au kukubali ofa nono ya kucheza Saudi Arabia.

Messi, ambaye atafikisha umri wa miaka 36 mnamo Juni 24, anakuwa mchezaji huru rasmi mkataba wake na Paris Saint-Germain ya Ufaransa utakapomalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Anaweza kucheza mechi yake ya kwanza Miami mwezi Julai au Agosti, kulingana na ripoti.

Inaripotiwa kuwa matatizo ya kifedha Barcelona yaliripotiwa kuwa yamekatiza hamu ya Messi kuungana tena na klabu ya Uhispania ya La Liga.

Saudi Arabia ilitoa kiasi cha dola milioni 400 kwa mwaka kucheza katika klabu ya Al-Hilal, ambayo ingemruhusu kuanzisha tena ushindani na Cristiano Ronaldo.

Messi ana mali huko Miami na amesema mara nyingi katika mwaka uliopita kwamba angependa kucheza nchini Marekani, vyombo vya habari vimeripoti.

Masharti ya makubaliano na Inter Miami hayako wazi kwa wakati huu, ingawa Messi bila shaka angeongeza kiwango cha juu zaidi katika historia ya MLS.

TRT Afrika