Kocha wa Morocco Walid Regragui na beki wa PSG ya Ufaransa, Achraf Hakimi, kwenye kikao chao cha waandishi wa kabla ya mechi yao dhidi ya Tanzania. Picha: Shirikisho la soka la Morocco.

Timu ya taifa ya soka ya Morocco imesema iko tayari kwa safari yake ya kufuzu kombe la dunia 2026 kwa mechi yake ya ufunguzi ikiwa mbioni kujihakikishia tiketi ya 2026.

"Tunajua itakuwa mechi ngumu sana, lakini tumejiandaa vizuri na tuko na motisha kama kawaida. Tumekuja hapa kusajili matokeo mazuri," kocha wa Morocco Walid Regragui alisema.

Timu hiyo itakutana na taifa stars ya Tanzania ambayo ilianza safari yake ya kufuzu kwa Kombe la dunia kwa kuifunga Niger 1-0 katika mchuano wake wa ufunguzi ugenini.

"Hatujioni kuwa timu spesheli kwa sababu ya kile tulichofanikiwa katika Kombe la Dunia Qatar."Tunaheshima kubwa kwa timu ya Tanzania, na tunajua wachezaji wake wanafurahi sana kutukabili, kwa sababu hii ni mechi ya mwaka kwao," alisema kocha wa Morocco Walid Regragui.

Timu hiyo, iliyokuwa kivutio cha wapenzi wa soka barani Afrika 2022 baada ya uhodari wake, wa kufika nusu fainali ya Kombe hilo la dunia nchini Qatar, imesema mechi yake dhidi ya Taifa stars ni kama fainali kwani macho yote yako kwao.

Kikosi cha Morocco kikiwa Kombe la Dunia 2026: Picha Getty

Hii ni kwa kuwa, mechi ya awali ya timu ya Morocco iliyopaswa kuchezwa Novemba 16 dhidi ya Eritrea ilifutwa baada ya Eritrea kujiondoa rasmi kutoka michuano hiyo ya kufuzu.

Kocha wa 'Simba wa Atlas' Walid Regragui amesema, "tunatarajia mchezo mgumu dhidi ya Tanzania na tunatarajia matokeo mazuri tu kama timu zingine zote ambazo zinatarajia kushiriki Kombe la dunia."

"Tumekuja hapa kupata matokeo mazuri. Ni mwanzo wa kufuzu na tunajua kwamba safari ni ndefu na inaanza kwa mechi hii. Tunafahamu jukumu ambalo linatusubiri na tunajua umuhimu wa mchuano huu," aliongeza kocha Walid.

"Ingawa Tanzania wana fursa ya kucheza mbele ya mashabiki wao wa nyumbani na kujawa na motisha na ujasiri wa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Niger, tunafahamu jukumu linalotusibiri na umuhimu wa mchuano huu," Aliongeza Regragui.

Morocco warudi nyumbani baada ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar

Beki Ashraf Hakimi, ambaye alikuwa na kocha Walid Regragui, ameongeza kuwa " mechi zote ni ngumu kuanzia sasa. Iwe Afrika au ulaya.

"Tanzania, ingawa iko nyumbani, na kuwa na nyota wake nahodha Mbwana Samatta na kikosi chenye umoja, sisi Morocco tunajiamini vilivyo bila wasiwasi au woga, kwani tumejiandaa vilivyo kujipa ushindi muhimu mechini, Hakimi amesema.

Morocco imekuwa ikiendelea na mazoezi yake nchini Tanzania siku chache kabla ya mechi yake dhidi ya wenyeji Taifa stars, ili kufahamu zaidi hali ya hewa na kujua zaidi kuhusu uwanja wa taifa wa Benjamin Mkapa, jijini Dar Es Salaam utakaoandaa mechi hiyo.

TRT Afrika