ronaldo

Cristiano Ronaldo (38), amekuwa mchezaji pekee duniani aliekuwa na michezo 198 tangu aanzie kuchezea taifa yake ya Ureno. Alifikia hio rekodi jana katika mechi yao na Luxembourg walipo shinda kwa mabao sita.

Ameibuka kama mchezaji wa kiume pekee aliecheza mechi nyingi kwenye soka ya kimataifa.

Ronaldo akiwa amenyakuwa tuzo ya kuheshimika ya Ballon d’Or mara tano aliweza kuvunja rekodi iliyo kuwa imeshikiliwa na mchezaji wa Kuwait, Bader Al-Mutawa akiwa na mechi 196.

Akichezea nchi yake ya Kuwait, Bader alishikilia hiyo rekodi tangu mwaka 2022. Ronaldo aliweza vunja rikodi hio wiki iliopita kwenye mechi yao na Liechtenstein katika kinyanganyiro cha kufuzu kombe la Ulaya EUROs.

Ronaldo ni kati ya wachezaji pekee walio wahi kunyakua tuzo ya Ballon d’Or mara tano na kunyanyua kombe la Champions League mara tano. Ronaldo ni mchezaji pekee aliyefunga mabao takribani 800 kwenye mechi 1100.

Ronaldo pia ni mwanamichezo pekee aliyefuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya jamii akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 513 kwenye Instagram pekee.

TRT Afrika