Rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa FIFA Gianni Infantino wakihudhuria mashindano ya soka ya 'Legends' na maafisa wa FIFA / Picha: Reuters

Wanasoka wakongwe zaidi ya 150 wanasubiriwa mjini Kigali nchini Rwanda mwezi Septemba katika Kombe la Dunia kati ya wachezaji wakongwe.

Takriban mechi 20 zitapeperushwa moja kwa moja kati ya tarehe 1 hadi 10 Septemba 2024 wakati wa mashindano hayo.

Miongoni mwa wanasoka wastaafu watakaoshiriki kutoka sehemu tofauti ulimwenguni watakaoshiriki ni pamoja na Jay Jay Okocha wa Nigeria, Samuel Eto’o wa Cameroon na Patrick Mboma.

Nyota wastaafu wa soka wengine wanaotarajiwa Rwanda katika michuano hiyo ni Ronaldihhno (Brazil), George Weah (Liberia), Gaizka Mendieta (Uhispania), Robert Pires (Ufaransa), Elizabeth Hooper Charmaine (Canada), Maicon Douglas Sisenando (Brazil), Patrick Mboma (Cameroon), Tsuneyasu Miyamoto (Japan), Jimmy Gatete (Rwanda) na wengineo kutoka mataifa mbalimbali.

Tayari Rwanda imesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuwa mwenyeji wa mashindano matatu mfululizo ya mashindano hayo kati ya 2024 hadi 2026.

Mnamo 2023, mashindano ya wachezaji wastaafu yalifanyika katika miji mbalimbali ikiwemo New York, Dubai, Berlin, London, Paris, Lagos, Johannesburg, Dar es Salaam na kuishia Abidjan.

Shindano hilo limeandaliwa na Serikali ya Rwanda, kupitia Wizara ya Michezo na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda.

TRT Afrika na mashirika ya habari