Chris Tibenda amemshinda Stori Embobe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika raundi ya kwanza ya pambano lao | Photo: Chris Tibenda

Mpiganaji wa MMA kutoka Tanzania Chris Tibenda amemshinda Stori Embobe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika raundi ya kwanza ya pambano lao la kilo 62 la MMA lililoandaliwa na Impact Championship, Lubumbashi Kusini mwa DRC usiku wa tarehe 8 Aprili.

Tibenda alishinda kupitia uwasilishaji (submission) katika raundi ya kwanza baada ya kumweka Embombe kwenye mkeka na kufululiza ngumi nyingi.

"Nina furaha sana kwa sababu nimeshinda na pia kwa sababu ninaweza kuwakilisha nchi katika kiwango cha kimataifa. Na bila klabu yangu, nisingekuwa hapa na kuwa na jasiri ambayo ilinipa." amesema Tibenda baada ya huo ushindi.

Pambano hilo lilikuwa kati ya 10 za usiku huo, lililojumuisha wapiganaji kutoka nchi tisa za Afrika waliokutana DRC zikiwemo Kenya, Rwanda, Burundi, Senegal, Angola na Kameruni kwa kutaja chache.

MMA bado ni mchezo unaokua lakini unapata mvuto mkubwa aeleza rais wa Impact Championship, ambaye huandaa hafla nchini DRC, Bwana Yad Mozer Mulunda.

“Mchezo sio mwiko na watu wanatazamia matukio na MMA inapata umaarufu mkubwa, watu wanaipenda na wanaiulizia sana. Watu wanataka kitu tofauti na tunabadilisha mchezo” amalizia kusema Mulunda.

MMA ni nini?

MMA au Mixed Martial Arts ni mchezo wa kupigana unaotumia mapigo huru au sanaa ya mapigo mchanganyiko.

Sanaa ya mapigo Mchanganyiko ni mchezo wa mapigano kamili unaozingatia kugonga, kugombana na mapigano ya ardhini, unaojumuisha mbinu za michezo mbalimbali ya mapambano kutoka duniani kote.

TRT Afrika haikubahatika kupata jibu kutoka kwa Story Embombe ambae hakupokea simu.

TRT Afrika