Akizungumza na Anadolu, Balozi Wijnands amesema "onesho hili linadhihirisha ushirikiano wetu mkubwa." / Picha: AA 

Balozi wa Uholanzi nchi Uturuki Joep Wijnands amepongeza uhusiano kati ya Ankara na Amsterdam.

Kauli yake imekuja wakati ubalozi wa Uholanzi uliandaa tamasha la muziki katika jimbo la Denizil lililoko magharibi mwa Uturuki, siku ya Jumapili. Tukio hilo lilienda sambasamba na uadhimishaji wa miaka 100 ya makubaliano ya urafiki kati ya Jamhuri ya Uturuki na Uholanzi.

Akizungumza na Anadolu, Balozi Wijnands alisema tamasha la pamoja linaonyesha kwamba "tuna ushirikiano mkubwa."

Akizungumzia kuleta pamoja makundi mawili ya muziki katika tamasha la pamoja katika mwaka maalum, balozi wa Uholanzi alisema: "Nadhani inaonesha ukweli kwamba tuna ushirikiano mkubwa. Sio tu kufanya biashara au kufanya kazi katika nyanja za kisiasa lakini kwenye muziki pia."

Orhun Orhon, mtiribu wa kusanyiko la Akademik Baskent, alisema kuwa tamasha la Denizli lilikuwa la 'kihistoria', akisisitiza kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili unadhihirishwa katika tamasha hilo.

Kwa upande wake, mpiga violin kutoka Hispania Anna Albero, alifurahishwa na tamasha hilo akisema kuwa maonesho kama hayo huleta watu pamoja.

'Uhusiano wa kidiplomasia kwa zaidi ya miaka 400'

Balozi wa Uholanzi alisema pia wametekeleza mradi wa kutafsiri vitabu vya mwandishi wa watoto wa Uholanzi Annie M.G. Schmidt katika lugha ya Kituruki.

"Tumewaalika wanafunzi kutoka Uholanzi kwenda Uturuki kuanza mchakato wa ujenzi," alisema.

Kuligana na mwanadiplomasia huyo, Uholanzi na Uturuki zimedumisha uhusiano wa kidiplomasia kwa zaidi ya miaka 400, toka enzi za dola ya Ottoman, na kwamba kuna urafiki na ushirikiano mkubwa kati yao hata leo. Pia alisisitiza umuhimu wa uhusiano wao kama washirika wa NATO.

Kuhusu uhusiano wa kiuchumi, balozi wa Uholanzi mjini Ankara alisifu kiwango cha biashara chenye nguvu na kinachokua kati ya Uturuki na Uholanzi.

"Uholanzi inajisikia fahari kuwa kati ya wawekezaji wakubwa nchini Uturuki. Tuna viwanda vya kiholanzi zaidi ya 3,000 nchini Uturuki," alisema.

Aliangazia uwepo wa jumuiya kubwa na yenye mafanikio ya Kituruki nchini Uholanzi, akibainisha kwamba raia wa Kituruki wa Kiholanzi wa kizazi cha pili, ambao wazazi wao walihamia Uholanzi katika miaka ya 1960, sasa ni wajasiriamali wenye mafanikio ambao wanawekeza Uturuki kutoka Uholanzi.

TRT Afrika