Kwa Nini Tetemeko la Ardhi la Morocco Lilisababisha Vifo Vingi?

Kwa Nini Tetemeko la Ardhi la Morocco Lilisababisha Vifo Vingi?

Tetemeko la ardhi la Morocco lililotokea 11 Septemba 2023 ambalo hadi sasa limeua watu zaidi ya 3000 lilisikika katika nchi tatu ambazo ni Algeria, Ureno na Uhispania. Wataalamu wa majanga wanasema, hili ni tetemeko kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha zaidi ya miongo mitano. Wataalamu wanasema, madhara ya tetemeko la ardhi yanaweza kuchangiwa na vigezo kadhaa na pia kuna aina tofauti ya matetemeko. Tetemeko la Morocco lilikuwa la kina kifupi ndio maana lilisababisha madhara makubwa zaidi. Lakini mbona tetemeko hilo liliua watu wengi kiasi hicho?