Jeshi la Iran limesema helikopta haikuonyeha athari ya kushambuliwa. / Picha: Reuters

Helikopta iliyokuwa imembeba aliyekuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi ilishika moto mara baada ya kugonga jabali na kuanguka, hakukuwa na dalili yoyote ya kushambuliwa, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti, vikiwanukuu wanajeshi wachunguzi wa ajali.

Taarifa kutoka kwa wafanyikazi wakuu wa vikosi vya jeshi wanaosimamia uchunguzi wa ajali hiyo ilisomwa kwenye runinga ya serikali mwishoni mwa Alhamisi. Taarifa ya kwanza kuhusu ajali hiyo haikutowa lawama za kushambuliwa kwa helikopta, lakini ilisema maelezo zaidi yatakuja baada ya uchunguzi zaidi.

Ajali hiyo siku ya Jumapili ilimuua Raisi, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo na watu wengine sita.

Raisi alizikwa kwenye kaburi la Imam Reza huko Mashhad siku ya Alhamisi.

Mfanyakazi Mkuu wa Jeshi la Iran ametoa ripoti ya awali kuhusu uchunguzi wa ajali hiyo.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa taarifa za kiufundi na za jumla na matokeo kuhusiana na ajali hiyo yamekusanywa na kutathminiwa, huku baadhi ya data zikihitaji muda zaidi kwa ajili ya tathmini, shirika rasmi la habari la Iran IRNA liliripoti Alhamisi.

Kulingana na tathmini ya awali, helikopta iliendelea na njia yake iliyopangwa bila kubadilisha njia. Rubani aliwasiliana na marubani wa helikopta nyingine mbili takriban dakika moja na nusu kabla ya ajali hiyo.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa hakuna athari zozote za risasi au uharibifu uliopatikana kwenye sehemu zilizosalia za helikopta hiyo na kwamba helikopta hiyo ilishika moto baada ya ajali hiyo.

Hali mbaya ya hewa na ukungu katika eneo hilo ilirefusha shughuli za utafutaji na uokoaji, eneo la ajali lilifikiwa asubuhi ya siku ya pili.

Hakuna hali za kutiliwa shaka

Ripoti hiyo inasema kwamba hakuna hali zozote za kutiliwa shaka zilizopatikana katika mnara wa kudhibiti mawsiliano na wafanyakazi wa ndege.

Matokeo ya mwisho ya uchunguzi yatashirikiwa mara tu utakapokamilika.

Mnamo Mei 19, Rais Raisi alihudhuria hafla ya uzinduzi wa bwawa kwenye mpaka wa Iran na Azerbaijan. Akirejea na Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian na baadhi ya maafisa, helikopta ya Raisi ilianguka.

Kwa ombi la Iran, Uturuki ilituma AKINCI, ndege isiyokuwa na rubani (UAV) kwa shughuli za utafutaji na uokoaji. Viratibu vya mabaki ya helikopta yaliyogunduliwa na UAV ya Uturuki yalishirikiwa na mamlaka ya Irani.

Timu ya Irani ilifika eneo hilo na kuripoti kuwa hakuna aliyenusurika.

Maelfu ya watu wamjumuika kuomboleza kifo cha Ebrahim Raisi huko Mashhad. /Picha: Reuters

Raisi alizikwa siku ya Alhamisi, kuhitimisha siku za ibada ya mazishi iliyohudhuriwa na umati wa waombolezaji, vyombo vya habari vya serikali viliripoti.

Mamia kwa maelfu walijumuika katika mji aliozaliwa wa Mashhad siku ya Alhamisi kumuaga Raisi kabla ya maziko yake kufuatia mikusanyiko katika miji ya Tabriz, Qom, Tehran na Birjand.

Siku ya Jumatano Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliongoza swala k ya kumuaga Raisi na wenzake.

Umati mkubwa kisha ulijumuika kutoka uwanja wa "Enghelab" (Mapinduzi) Square hadi uwanja wa "Azadi" .

TRT World