Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha mistari mirefu ya vijana wakiwa wamejifunga pingu na kuvaa shati jeusi zenye maneno "Not In Our Name" na "Cease Fire Now" yakiwa yamechapishwa kwa rangi nyeupe. / Picha: AFP

Mamia ya watu wametiwa mbaroni wakati polisi walipotawanya maandamano makubwa ya wakazi wengi wa Wayahudi wa New York ambao walikuwa wameteka jumba kuu la kituo cha Grand Central kupinga mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya Gaza, polisi na waandalizi walisema.

Idara ya Polisi ya New York ilisema takriban watu 200 wametiwa mbaroni siku ya Ijumaa, huku waandalizi wa maandamano hayo wakiweka idadi hiyo kuwa zaidi ya waandamanaji 300 wanaopinga Uzayuni.

Picha kutoka eneo la tukio zilionyesha misururu mirefu ya vijana wakiwa wamejifunga pingu na kuvaa shati jeusi zenye maneno “Not In Our Name” na “Cease Fire Now” (Kumaanisha : 'Sio kwa Jina letu'' na '' Komesha vita mara moja'') yakiwa yamechapishwa kwa rangi nyeupe.

Kikao hicho kikubwa kiliitishwa na kundi la Jewish Voice for Peace-New York City, ambalo lilisema maelfu ya wanachama wake walihudhuria maandamano hayo, wakizuia njia kuu ya kituo cha reli cha kati cha jiji hilo.

Picha zilionyesha uwanja huo ukiwa umejaa waandamanaji ambao waliinua mabango yaliyoandikwa "Wapalestina wanapaswa kuwa huru" na "Waombolezeni wafu, wapiganie kufa kupona walio hai."

Waandaaji walitaja kuketi kwa amani "uasi mkubwa zaidi wa kiraia katika jiji la New York kuwahi kutokea katika miaka 20."

'Maisha ya Wapalestina na Waisraeli yanaingiliana'

Viongozi wa kidini wa Kiyahudi walizindua tukio hilo kwa kuwasha mishumaa ya Shabbat na kukariri sala ya Kiyahudi ya wafu, inayojulikana kama kaddish.

"Wakati Shabbat kwa kawaida ni siku ya mapumziko, hatuwezi kumudu kupumzika wakati mauaji ya halaiki yanajitokeza kwa majina yetu," alisema Rabbi May Ye, katika taarifa iliyotolewa na waandalizi.

"Maisha ya Wapalestina na Waisraeli yameunganishwa, na usalama unaweza tu kutoka kwa haki, usawa, na uhuru kwa wote," rabi huyo alisema.

Mzozo huo uliongezeka sana baada ya tawi la kijeshi la Hamas kufanya uvamizi ambao haujawahi kushuhudiwa nchini Israel tarehe 7 Oktoba kwa kurusha maelfu ya maroketi na kutuma mamia ya wapiganaji katika miji na makazi ya Israel.

Israel ilijibu kwa mashambulizi ya angani na mizinga bila kukatizwa kwenye eneo lililozingirwa na kuua Wapalestina wasiopungua 7,326, wakiwemo zaidi ya watoto 3,000. Takriban Waisrael 1,400 waliuawa katika harakati za Hamas.

Wakaazi milioni 2.3 wa Gaza wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji, na dawa kutokana na mashambulizi makubwa ya anga ya Israel na kuzingirwa kabisa kwa eneo hilo.

Siku ya Ijumaa, Israel iliongeza kasi ya mashambulizi yake baada ya kuondosha mtandao na mawasiliano katika Gaza iliyozingirwa, na kwa kiasi kikubwa kuwakataza idadi ndogo ya Wapalestina kupata mawasiliano kati yao na ulimwengu wa nje.

"Habari hii kukatizwa kunahatarisha kuficha ukatili mkubwa na kuchangia kutokuadhibiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu," Human Rights Watch ilisema katika taarifa.

TRT World