Rais wa Chama cha Soka Zambia Andrew Kamanga amekamatwa huku akikabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa fedha za umma na Utakasishaji. Picha: COSAFA

Rais wa Chama cha Soka Zambia Andrew Kamanga ametiwa nguvuni na mamlaka ya kukabiliana dawa za kulevya pamoja na ubadhirifu wa pesa za umma DEC.

Kamanga anatuhumiwa kwa madai ya ubadhirifu wa fedha za umma na utakasaji wa pesa.

Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Reuben Kamanga, pia amekamatwa.

Shtaka dhidi yake ni madai ya kufyonza fedha zilizotengwa kwa chama cha Soka cha Zambia na serikali yake ili kufidia gharama ya malazik wa watu wawili waliosafiri kwenda Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.

Rais huyo anatuhumiwa kutumia fedha za serikali kuwawezesha ndugu na rafiki zake, kusafiri kushuhudia Kombe la Afcon, licha ya wawili hao kutokuwa maafisa wa chama cha soka cha Zambia, FAZ.

Sasa Kamanga anasubiri kufunguliwa kesi rasmi baada ya kukamatwa, kwani ameachiliwa kwa dhamana.

Iwapo atahukumiwa, atakuwa ni rais wa tatu wa shirikisho la soka barani Afrika kufungwa kufuatia kukamtwa kwa rais wa Chama cha Soka nchini Tunisia Wadi Al Jari na Will Bavieux Touré wa Mali Oktoba na Agosti mwaka 2023.

TRT World