Watafiti waligundua kuwa machapisho ya matusi ya mitandao ya kijamii yalijumuisha hasa aina za chuki, ubaguzi na unyanyasaji wa kihisia, hasa kwa wanariadha wa kike / Picha: X - Eliud  Kipchoge

Akili Bandia itatumika kwa mara ya kwanza kuwalinda wanariadha dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni.

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imetangaza kuwa huduma hiyo mpya ya ufuatiliaji inayoendeshwa na AI itawalinda wanariadha na maafisa dhidi ya matumizi mabaya ya mtandaoni katika Michezo ya Olimpiki na ya Walemavu ya Paris 2024 msimu huu wa joto.

''Mfumo unaoendeshwa na AI utafuatilia maelfu ya akaunti kwenye majukwaa yote makubwa ya mitandao ya kijamii na katika lugha zaidi ya 35 kwa wakati halisi,'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

IOC ilisema mfumo huo ulifanyiwa majaribio wakati wa Wiki ya Michezo ya Olimpiki mnamo 2023, ikichambua zaidi ya machapisho 17,000 ya umma, ikiripoti ujumbe 199 zinazoweza kuwa za matusi kutoka kwa waandishi 48 zinazolenga akaunti kutoka kwa seti ya utafiti ya wachezaji 122 na akaunti mbili rasmi za IOC.

Hii ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa kupunguza unyanyasaji wa wanariadha wa kulipwa ambao unasemekana kuongezeka kupita kiasi.

Utafiti ulioagizwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), ulionyesha kuwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayolenga wanariadha yameongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni huku hadi theluthi moja ya machapisho sasa yakiwa na maudhui hasi yanayowalenga wanamichezo.

Eliud Kipchoge alitukanwa mtandaoni

Watafiti waligundua kuwa machapisho ya matusi ya mitandao ya kijamii yalijumuisha hasa aina za chuki, ubaguzi na unyanyasaji wa kihisia, hasa kwa wanariadha wa kike.

Miongoni mwa wanariadha mashuhuri waliolalamikia kunyanyaswa mtandaoni ni Eliud Kipchoge.

Katika utafiti uliofanywa na Kamati hiyo ya Olimpiki juu ya unyanyasaji wa wanariadham mtandao wa X, zamani twitter ndio hutumika zaidi. / Picha: X - Eliud Kipchoge 

"Nilishtuka kwamba watu kwenye mitandao ya kijamii wanasema 'Eliud anahusika katika kifo cha kijana huyu'," Kipchoge aliambia BBC Sport Africa. "Hiyo ilikuwa habari yangu mbaya zaidi kuwahi kutokea maishani mwangu.

Kiptum aliuawa katika ajali ya gari mnamo Februari akiwa na umri wa miaka 24 tu, miezi michache tu baada ya Mkenya huyo kuvunja rekodi ya dunia ya mwenzake Kipchoge mjini Chicago.

Kiptum alionekana kuwa tayari kupunguza rekodi zaidi na kupinga ubabe wa Kipchoge kwenye mchezo huo.

ELiud anasema, alipokea kila aina ya matusi na unyanyasaji huku akilaumiwa imma kuhusika kwa kifo cha mwanariadha huyo au wengine wakimkosoa kutokuwa na huruma ya kutosha kufuatia kifo cha Kiptum.

"Cha kuhuzunisha ni kuwa walinilenga sio mimi tu bali pia familia yangu,'' aliongeza Kipchoge.

Utafiti kwa Muhtasari

Katika utafiti uliofanywa na Kamati hiyo ya Olimpiki juu ya unyanyasaji wa wanariadha mtandao wa X, zamani twitter ndio hutumika zaidi.

  • X (zamani Twitter) ndicho kilichopendelewa kwa watumizi, ikichukua takriban 90% ya unyanyasaji uliogunduliwa, ongezeko la 500% ikilinganishwa na 2022.

  • Unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi ulijumuisha zaidi ya theluthi moja ya unyanyasaji wote, ongezeko la 14% kutoka 2022

  • Wanariadha wa kiume walikabiliwa na ongezeko la unyanyasaji, huku mgawanyiko wa kijinsia wa unyanyasaji ukiwa 51% ukiwalenga wanaume na 49% ukilenga wanawake.

  • Wanariadha wawili kati ya 1344 waliofuatiliwa walipokea 44% ya unyanyasaji wote uliohesabiwa kati yao

Wanariadha 15000 watafaidika

Kwa mujibu wa OIC, mradi huu wa Akili Bandia utasaidia kamati hiyo kuelewa vyema changamoto wanazokabiliana nazo wanariadha kuhusiana na matumizi mabaya ya mtandaoni, na kuiwezesha kuimarisha zaidi ulinzi wa wanariadha katika matukio yajayo.

Mfumo huo wa ufuatiliaji wa mtandaoni utatolewa kwa wanariadha 15,000 na maafisa zaidi ya 2,000 katika Michezo ya Olimpiki na Walemavu.

TRT Afrika