#KOD68 : Ramadan / Photo: AFP

Na Halima Umar Saleh

Raia wa Nigeria wamekuwa wakielezea wasiwasi wao juu ya uhaba wa sarafu huku waislamu wa nchi hiyo wakijiandaa kuanza mfungo wa Ramadhani.

Wengi wa wale amabo ni waislamu hutumia pesa nyingi zaidi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kununua vhakula na vitu vingine muhimu.

Mwezi Oktoba mwaka jana, Benki kuu ya Nigeria ilianzisha sera ya kubadilisha madhehebu fulani ya naira na noti mpya za sarafu zilizoundwa.

Serikali ilisema hatua hiyo ilichukuliwa ili kukabiliana na uhalifu ikidai kuwa fedha nyingi zilikuwa mikononi mwa watu wachache wafisadi.

Lakini hii imesababisha uhaba mkubwa wa pesa taslimu, na kuacha mamilioni ya watu wasiweze kupata noti za zamani na mpya na hivyo kufanya miamala ya biashara kuwa ngumu sana.

Upungufu wa noti za benki haswa wakati huu umekatisha tamaa waumini wengi wa Kiislamu ambao kwa kawaida hutumia pesa nyingi wakati wa Ramadhani.

“Ninaipenda Ramadhani”

Bwana Tijjani, mkaazi wa mashambani katika jimbo la Bauchi, kaskazini mashariki mwa Nigeria, anasema tatizo hilo linaathiri watu wengi wanaoishi katika maeneo ya mbali.

“Ninaipenda Ramadhani na nina hamu sana ya kuanza mfungo lakini jambo langu kuu ni jinsi ya kupata pesa za kutosha kila siku kununua vyakula vya msingi vya kutoa kama sadaqah (sadaka) kwa wengine," alikashifu Malam Tijjani, katika mahojiano na TRT Afrika.

“Kwa hivyo unadhani tutafurahiaje maisha yetu katika mwezi huu mtukufu? Je, tunawezaje kuuza na kununua vitu muhimu?”

“Sijaweza kununua chochote katika maandalizi ya Ramadhani hii kwa sababu ya matatizo ya uhamisho wa fedha ambayo nimekuwa nikikabiliana nayo,” anasema.

Wakati wa Juma’at Khutba yao ya hivi majuzi, viongozi wengi wa dini ya Kiislamu waliitaka benki kuu kutoa noti zaidi za naira kwani miezi ya Ramadhani ilikuwa inakaribia.

Profesa mashuhuri, Jibrin Ibrahim siku ya Jumatano, aliandika katika mtandao wake wa tweeter kuhusu uhaba unaoendeleaa ki kumuuliza Rais Muhammadu Buhari na gavana wa benki kuu ya taifa ni lini changamoto hii itaikwisha.

Watu wengi walituma tena na kujibu ujumbe wa Profesa Jibrin, wakielezea hofu yao kuhusu kuanza mfungo wa Ramadhani "katika hali hii mbaya."

Wanawake wanaaminika kuwa mstari wa mbele katika kuendesha shughuli za familia hasa kwa kupanga bajeti ya chakula au kutumia wakati wa mfungo.

Wengi wao waliozungumza na TRT Afrika kutoka maeneo ya vijijini na mijini wanasema wanapambana na hali ya wasiwasi inayoongezeka kuhusu jinsi ya kuongeza bidhaa kwa maduka yao kabla ya kuanza mfungo.

Fadila Bashir, mkaazi wa jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria, anaelezea hali katika miji kama "bora zaidi kuliko katika maeneo ya vijijini".

"Angalau tuna akaunti za benki, upatikanaji wa uhamisho, POS na ATM, sio kama watu wetu wa vijijini. Walakini, mtandao wa kufikia mitindo ya kifedha unaweza kumfanya mtu awe wazimu,” mmoja anasema

“uhamisho wa pesa kutoka benki moja hadi ingine unaendelea kushindikana, huduma za mashine ya ATM na mashine za malipo ya kadi imekuwa changamoto pia. Hakuna atakayekupa hata mkate bila kupokea pesa yake kwanza. Kuchanganyikiwa huku pekee kunaweza kusababisha shinikizo la damu yako na kukufanya uwe na hasira,” aliongeza.

Samira Ciroma anasema anatatizika kununua nyama ambayo inahitajika na familia yake kama sehemu ya vyakula vya iftar.

"Wauzaji wa nyama hawakubali kutumiwa pesa kwa akaunti za benki au kutumia mashine ya malipo ya kadi. Hiyo inamaanisha kuwa Ramadhani hii itakuwa tofauti kabisa na ngumu.”

Aliyu Musa,baba wa watoto saba na mke mmoja, ana wasiwasi kuhusu jinsi maisha yanavyoendelea kuwa magumu,

"Nina pesa kwenye akaunti yangu ya benki lakini zinaonekana kama sio zangu. Siwezi kufanya aina yoyote ya shughuli kwani inazidi kuzorota. Ramadhani inaanza kesho, tunahitaji chakula cha mlo wa kabla ya alfajiri (Sahur), lakini ninawezaje kununua vyakula?”

"Nimekuwa nikijaribu kuhamisha pesa kwa akaunti ya benki tangu siku tatu zilizopita kwa muuzaji duka katika mtaa wangu ambaye alinipa vitu kwa mkopo lakini sikuweza na tayari nimefikia kikomo chake.”

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanahofia kuwa hali hii inaporomosha uchumi na wajasiriamali wadogo na wa kati.

Waislamu wengi nchini wanaamini kuwa Ramadhani ya mwaka huu inaweza kuwa ngumu zaidi kuliko ile waliyoipata mnamo 2020 wakati wa janga la Uviko 19 wakati wa kufuli.

TRT Afrika