Gianluca Scamacca alifunga mara mbili na kuiduwaza Liverpool nyumbani kwao Anfield katika mechi ya kwanza ya Kombe la Ligi la Ulaya./Picha: Reuters  

Mabao mawili ya Gianluca Scamacca wa Atalanta yalitosha kuididimiza Liverpool kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Ligi la Ulaya, siku ya Alhamisi.

Matokeo hayo yametia dosari matumaini ya Liverpool kutwaa mataji matatu katika msimu huu na wa mwisho kwa meneja Jurgen Klopp ndani ya Anfield.

Timu hiyo kutoka Italia ilipata bao la kwanza katika dakika ya 38 kupitia kwa Scamacca baada ya shuti lake la chini chini kumpita mlinda mlango Caoimhin Kelleher.

Ilimlazimu Klopp kufanya mabadiliko na kuwaingiza Mohamed Salah, Dominik Szoboszlai na Andy Robertson katika kipindi cha pili. Hata hivyo, Scamacca alitupia bao la pili kufuatia krosi nzuri ya Charles De Ketelaere katika dakika ya 60 ya mchezo.

Mchezo huo unaweza ukawa wa mwisho ndani ya Anfield kwa kocha Klopp katika ngazi ya Ulaya./Picha: Reuters

Mario Pašalić alishindilia msumari wa mwisho kwenye sanduku la Liverpool, dakika saba kabla ya mchezo.

Mwaka 2020, timu hizo zilikutana katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Atalanta ikiifunga Liverpool 2-0 katika uwanja wa Anfield.

Mchezo huo unaweza ukawa wa mwisho ndani ya Anfield kwa kocha Klopp katika ngazi ya Ulaya.

TRT Afrika
AP