Joshua Cheruiyot Kirui amekuwa akisambaza picha zake wakati wa kupanda milima tofauti. / Picha: Joshua Cheruiyot Kirui/ Instagram

Waandalizi walisema kuwa mwili wa Kirui ulipatikana mita chache kileleni mwa Mlima Everest.

"Alikuwa na dhamira ya ujasiri kufika kileleni bila oksijeni ya ziada na aliandamana na mpanda milima wa Nepal Nawang, ambaye hatima yake bado haijulikani," ilisema ripoti ya Alhamisi ya tovuti ya habari ya wapanda milima ya Nepal Everest Today.

Kirui, mfanyakazi wa benki ya Kenya Commercial Bank, alipotea akiwa na muongozaji wake Nawang.

Maafisa kutoka Seven Summit Treks (SST), kampuni ya wapanda mlima iliyoko Kathmandu, Nepal, waliripotiwa kupoteza mawasiliano na Kirui na mungozaji wake katika eneo la Bishop Rock, lililoko kwenye mwinuko wa mita 8,000.

Everest ndio mlima mrefu zaidi duniani, wenye mwinuko wa mita 8,848.86 juu ya usawa wa bahari. Uko katika mpaka wa China na Nepal.

Joshua Cheruiyot Kirui alitaka kuwa mwafrika wa kwanza kupanda Mlima Everest bila oksijeni ya ziada.

Joshua pia aliwahi kuupanda Mlima Kenya na Mlima Kilimanjaro bila ya changamoto yoyote.

TRT Afrika