Kamala Harris in Ghana

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, yupo katika ziara ya wiki moja barani Afrika, iliyo anzia nchini Ghana.

Hata hivyo, ziara yake ilipelekea kuibuka kwa kwa picha ya video iliyo sambaa mtandaoni, ikionyesha Vikosi vya Usalama vya Marekani vikichukua udhibiti wa ukaguzi wa usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ghana.

Baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii walionyesha kuhamaki juu ya ushiriki wa Idara ya Usalama katika ukaguzi wa usalama, na wengine wakimkosoa Rais wa Ghana kwa kuruhusu hilo.

Wengine walipongeza ufanisi wa wanausalama hao, ambao walihakikisha watu wanaoingia katika jumba hilo walifanyiwa ukaguzi kwa usahihi kabla ya kuwasili kwa Makamu wa Rais.

Katika jukwaa la Twitter, mtumiaji Kofi Asamoah alisema "Aibu ilioje! Je! Hivi ndivyo vikosi vyetu vya usalama pia vinachukua udhibiti pindi Rais wetu anaposafiri nje ya nchi?"

Je utaratibu hasa ni upi?

Unaweza sema inamaana viongozi wa kutoka nje hawana imani na ulinzi wa waafrika? Lakini Adam Bonaa rais wa taasisi ya ulinzi ghana anafafanua.

"Ulinzi huu huandaliwa kabla ya ziara, na mipango maalum hufanywa kwa ajili ya mhusika huyo. Wamarekani watatumia kila kinachohitajika kulinda watu kama hao," anaeleza Adam Bonaa anafafanua

"Askari kanzu hutumika kwa uchunguzi, na ufungaji vifaa vya upelelezi ambapo hufanyika miezi kadhaa kabla. Wanatumwa kuandaa njia ya timu kamili ya usalama, ambayo hutangulia wiki kabla ya Makamu wa Rais au nchi nyingine yenye nguvu kama hii," anaelezea TRT Afrika.

Taarifa za msingi hutolewa kwa watu muhimu ili wajue kwamba umma utafanyiwa ukaguzi katika sehemu ambapo mgeni wa heshima atakuwa, na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Hoja ndani ya manung’uniko

Video hio iliibua mjadala mkali mtandaoni, ambapo baadhi ya watumiaji walilaani walichokiona kama ukoloni mamboleo na wengine wakipongeza matumizi ya ujasusi na teknolojia.

Kwa Makamu wa Rais wa Marekani anayetembelea ukanda kama huu, huku akitokea nchi ambayo imehusika katika mivutano na vurugu zaidi ulimwenguni, ni lazima kuwe na ulinzi mkali nyuma yake. Hatua kama hizi za Marekani zinahitajika kuhakikisha kwamba mapungufu ya kiusalama hayajitokezi.

Mtumiaji mwingine wa Twitter, Ghana Nyobi anasema “Kama viongozi wa Marekani wangekuwa watu wazuri na wapenda amani hawangelazimika kujiwekea ulinzi mzito kama huo kwa mtu mmoja. Wameumiza watu na nchi nyingi sana kiasi kwamba hawawezi kutembelea nchi yenye amani kama Ghana bila ulinzi mkali.”

"Utaratibu wa ulinzi, kwa mfano, kwa mkuu wa Kanisa Katoliki la Roma, unaweza usifanane na wa nchi kama Marekani kwa kupima vigezo vingi. Hata katika nchi kama Ghana, usalama ungekuwa tofauti kabisa na huu.

Hata hivyo, Makamu wa Rais alifika wakati wa sherehe huko Accra Jumapili iliyopita ambako ndio kilikuwa kituo chake cha kwanza katika ziara yake ya Afrika. Makamu wa Rais alikaribishwa uwanja wa ndege na watoto wa shule.

Ziara yake inakuja wakati Marekani ikikabiliwa na tukio jingine la mashambulizi ya risasi katika shule moja wiki hii, na kufanya jumla ya watu waliouawa kwa kupigwa risasi kufikia 130 katika mwaka huu pekee.

Mtumiaji wa Instagram Wema Adewale anasema "Natumaini Waghana nao wataw apekua Wamarekani jinsi hii watakapoenda ziarani. Upuuzi gani huu?"

“Kuna viwango mbalimbali vya usalama vinavyozingatiwa kabla na baada ya ugeni kuwasili. Kwa kawaida, Wamarekani wanataka kusimamia wenyewe baadhi ya maeneo muhimu ya ulinzi huku wakiwahusisha polisi wenyeji kila hatua. Na hii inafanyika zaidi kabla, wakati na hata baada ya Makamu au hata Rais kuondoka," anaelezea Bonaa.

Hii inafanyika wakati wa kujadili Mahusiano ya Kimataifa na hatua za Usalama wa Kimataifa, Bonaa anasisitiza.

Ziara ya Harris barani Afrika inakuja wakati Marekani ikitaka kurekebisha uhusiano na Afrika baada ya kuzorota wakati wa utawala wa Trump. Marekani ilizindua mkakati wa Afrika mwezi Agosti mwaka jana wa kuboresha demokrasia barani Afrika.

Licha ya mijadala kuhusu ukaguzi ulio simamiwa na wageni, ziara ya Harris nchini Ghana ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Makamu wa Rais sasa yuko Tanzania kama sehemu ya ziara yake ya nchi tatu za Afrika, na baada ya hapo ataelekea Zambia.

TRT Afrika