Na Colettha Wanjohi
Huku kikosi cha Afrika cha kulinda amani nchini Somalia, ATMIS, kikitimiza mwaka mmoja, Umoja wa Afrika umepongeza nchi zinazochangia wanajeshi katika mchakato huu wa kulinda amani kwa kusaidia Somalia katika jitihada zake za mpito.
ATMIS ina jukumu la kuhamisha majukumu ya usalama kwa vikosi vya usalama vya Somalia.Kazi ya kikosi hiki imebadilishwa kutoka kwa ile awali ya kulinda amani nchini Somalia, AMISOM, ujumbe wa Umoja wa Afrika ulioongoza katika kulinda amani nchini Somalia tangu 2007.
"Tunataka kutambua na kuheshimu utumishi wa wanajeshi wa Umoja wa Afrika, ambao wengi wao wamejitolea kabisa katika mfumo hiyo ya ushupavu ya kurejesha amani na usalama,” mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahammat anasema katika taarifa yake.
ATMIS yenye wanajeshi 18,586, imetekeleza majukumu yake mwaka jana kwa msaada wa washirika wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Uturuki, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Falme za Kiarabu na Marekani. Wanajeshi 2000 wa kwanza kutoka kikosi hiki wamepagwa kuondoka kufikia 30 Juni 2023.
Je,tunajua nini kuhusu Ujumbe wa mpito wa Afrika nchini Somalia, ATMIS?
Oparesheni ya kikosi cha ATMIS ilianza tarehe 1 Aprili 2022, kwa idhini ya Umoja wa Afrika na kupewa mamlaka na Umoja wa Mataifa.
Mamlaka yake ni Pamoja na :
- kudhalilisha wagaidi wa Al Shabaab na vikundi vingine vya kigaidi
- kutoa usalama kwa vituo vya idadi ya watu na kufungua njia kuu za usambazaji
- kuendeleza uwezo wa vikosi vya usalama vya Somalia ili kuviwezesha kuchukua majukumu ya usalama ifikapo mwisho wa kipindi cha mpito, yaani, Desemba 2024.
- Kuunga mkono juhudi za amani na upatanisho za Serikali ya shirikisho la Somalia
- Kusaidia kukuza uwezo wa taasisi za usalama, haki na mamlaka ya ndani ya Serikali ya shirikisho la Somalia na nchi wanachama wa shirikisho
- Kuondoka kwa ATMIS kutoka Somalia kunatarajiwa Desemba 2024