Waziri wa Uingereza Rishi Sunak amesema waomba hifadhi watasafirshwa Rwanda baada ya uchaguzi. /Picha: Reuters

Rishi Sunak amesema cha cha upinzani cha Conservative kikishinda uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika Julai tarehe 4, huenda kikasitisha mpango wa kusafirisha waomba hifadhi nchini Rwanda.

Chama cha upinzani hapo awali kilisema iwapo watashinda uchaguzi huo watasimamisha mpango wa kusafirisha waomba hifadhi.

Akizungumza katika hafla ya kampeni siku ya Alhamisi, Sunak alisema mpango huo ndio utakua msingi wa kinyang'anyiro cha kisiasa na uchaguzi ujao. Mnamo Aprili, alikuwa ameahidi kuwa safari za ndege za kusafirsha waomba hifadhi zingeanza baada ya wiki 10 hadi 12. Huku waomba hifadhi wengi wameanza kukamatwa ili kusafirishwa Rwanda.

"Tumeanza kuwakamata watu, safari za ndege zimepangwa mwezi wa Julai, viwanja vya ndege viko kwenye hali ya kusubiri, wasindikizaji wako tayari, wahudumu wa kesi wapo imara, kwa hivyo ikiwa nitachaguliwa tena kuwa waziri mkuu wenu, ndege hizo zitaenda Rwanda,” Sunak alisema.

Mpango wa kufurushwa kwao umekuwa sera kuu kwa Sunak tangu aingie madarakani Oktoba 2022. Ameendelea kuutetea hata baada ya Mahakama ya Juu ya Uingereza kuamua mpango huo kuwa kinyume cha sheria kwa misingi kwamba Rwanda haiwezi kuchukuliwa kuwa nchi salama.

Kwa upande wake, kiongozi wa chama cha Labour Keir Starmer aliapa mapema mwezi huu kutupilia mbali mpango huo, ambao tayari umegharimu mamia ya mamilioni ya pauni, "mara moja" atakapoingia madarakani.

Starmer amesema, kupigana na shida ya wakimbizi haramu kuingia Uingereza, atahikisha mpaka wa Uingereza umedhibitiwa.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika