Kanisa la Afrika Kusini lafanya harusi kubwa sana ya Pasaka na wanandoa 800 | Picha: Reuters

Zaidi ya wanandoa 800 walifunga ndoa siku ya Jumapili ya Pasaka katika mojawapo ya sherehe kubwa zaidi za harusi nchini Afrika Kusini tangu janga la UVIKO-19.

Kanisa la International Pentecostal Holiness Church hubariki ndoa za wake wengi, ambazo ni za kawaida katika baadhi ya jumuiya za Kiafrika, na kanisa linasema kuwa zimeidhinishwa na Biblia.

Misa za Harusi hufanyika mara tatu kwa mwaka - wakati wa Pasaka, mnamo Desemba, na pia wakati wa maadhimisho ya Septemba ya kuanzishwa kwa kanisa mnamo 1962.

Lebogile Mamatela, 38, mfanyakazi wa serikali ambaye alikua mke wa pili wa baba wa mtoto wake siku ya Jumapili, aliliambia shirika la habari la Reuters baada ya sherehe: "Ni siku maalum, nina furaha sana. Ninathamini sana wakati huu wa kuwa. sehemu ya familia ya Mahluku. Ni hisia nzuri."

Mume wake mpya, Roto Mahluku, 40, alijiunga na kanisa hilo mwaka wa 1993 na kuoa mke wake wa kwanza, Ditopa Mahluku, miaka 16 iliyopita. Wana watoto watatu.

Ditopa, mwenye umri wa miaka 37, alisema ndoa ya pili ya mume wake "inatimiza kile ambacho Mungu ametuumbia, kutimiza andiko linalosema wanawake watakuwa wakiegemea kwa mwanamume mmoja".

Wake wapya walivaaa mavazi ya kupendeza kwenye sherehe hiyo katika sherehe la International Pentecost Holiness Church la Jerusalem, kilomita 100 kaskazini mwa Johannesburg. Maharusi wa mara ya kwanza walivaa nguo nyeupe za kitamaduni.

Sherehe hizo ziliondoa mzozo wa muda mrefu kuhusu uongozi wa kanisa hilo lenye waumini takribani milioni tatu na kuifanya kuwa miongoni mwa mikutano mikubwa nchini Afrika Kusini.

Vita vya urithi kati ya ndugu watatu vilianza baada ya kifo cha kiongozi wa kanisa hilo Glayton Modise mnamo 2016.

Mwaka 2020 watu watano waliuawa kwa kupigwa risasi katika mkutano mwingine wa kanisa hilo, lakini mahakama mwaka jana ilitupilia mbali kesi dhidi ya washtakiwa 42.

Ulinzi ulikuwa mkali katika sherehe ya Jumapili, ambayo ilisimamiwa na walinzi wenye silaha na vifaa vya kugundua chuma vilitumiwa kuwachunguza waumini.

TRT Afrika na mashirika ya habari