Mcheza taekwondo kwa walemavu Bozteke wa Uturuki./Picha: AA   

Licha ya mcheza taekwondo maalumu ya walemavu kutoka Uturuki, kuvunjika kidole katikati ya pambano lake dhidi ya mpinzani wake wa Israeli, Mahmut Bozteke ameshinda pambano hilo na kuliita sauti ya watu wa Palestina wanaoteseka mjini Gaza.

Bozteke alifanikiwa kushinda pambano hilo la nusu fainali la uzani wa kilogramu 63, na kunyakua medali ya fedha katika michuano ya ubingwa wa Ulaya, yaliyofanyika nchini Serbia, Mei 10.

Licha ya kushindwa kushiriki hatua ya fainali ya pambano hilo, bingwa huyo wa Ulaya wa taekwondo maalumu kwa walemavu anaamini kuwa ushindi wake ni ushindi dhidi ya Israeli.

“Niligundua natoka damu kwenye glovu zangu, lakini nikaendelea kupambana,” anasema Bozteke.

“Wakati wa mapumziko niligundua kuwa nimeumia katika ya vidole vyangu,” alisema.

Bozteke aliongeza kuwa kukabiliana na mpinzani wa Israeli kwenye nusu fainali kulimtia motisha licha ya jeraha hilo.

“Huwezi kuhisi maumivu kwa wakati huo. Lengo lako ni kushinda tu na kumaliza mchezo huo,” anasema Bozteke.

“Na ndio maana sikuondolewa kwenye mpambano huo,” alisema. “Kwa sasa Israeli inatekeleza mauaji ya kimbari. Dunia nzima inapuuzia hilo. Tunapambana ulingoni kama sauti ya Wapalestina.”

“Tutakuwa mahakamani na hatotuwapa Waisraeli nafasi yoyote. Madhali tuko hapa, hawatafanikiwa,” alisema.

Kusaka medali ya dhahabu kwenye michezo ya mwaka 2024

Bozteke alipuuzia jeraha hilo na kumaliza mechi kabla ya kupokea matibabu.

“Baada ya mechi, timu za madaktari ziliingilia kati na ikabidi nipelekwe hospitali. Sikuweza kufuzu katika mechi ya fainali na hivyo kuishia na medali ya fedha,” alisema.

Licha ya kukaribia ubingwa wa Ulaya kwa mara ya tano mfululizo, Bozteke aliridhika na medali ya fedha.

Akizungumzia mafanikio yake ya awali, ambayo ni pamoja na kumaliza katika nafasi ya tatu katika Olimpiki yake ya kwanza, Bozteke alikiri kutoridhika na kushindwa kuendelea na mfululizo wa ushindi Ulaya.

"Hii ilikuwa mara ya kwanza kwangu jambo kama hili kunitokea. Sikuwahi kujiondoa kwenye mashindano yoyote hapo awali. Ingekuwa ni ubingwa wangu wa tano mfululizo wa Ulaya. Nimekuwa bingwa wa Ulaya tangu 2019,” alisema.

Hata hivyo, Bozteke amejiwekea malengo ya kushinda medali ya dhahabu katika michezo ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Paris, Ufaransa.

"Tuna mchuano muhimu zaidi mbele yetu, michezo ya walemavu. Tunaamini tutafanikisha mambo makubwa hatua hii,” alisema.

TRT Afrika