Rais Erdogan amesema shinikizo kwa Israeli litaendelea hadi pale ukatili dhidi ya Wapalestina utasitishwa. /Picha: A A

Akizungumza katika mkutano wa Bodi ya Mahusiano ya Kiuchumi ya Kigeni (DEIK) mjini Istanbul Jumamosi, Erdogan alikuwa wazi kabisa kuhusu kile ambacho kimekuwa kikitokea Gaza tangu Oktoba 7, 2023.

"Tunaweka njia zetu za mawasiliano wazi katika jumuiya yetu ya wafanyabiashara, katika mchakato wa kutekeleza uamuzi wetu wa kusimamisha shughuli za kibiashara ili kuilazimisha Israel, ambayo imeua mashahidi karibu 36,000 wasio na hatia huko Gaza, kusitisha mapigano," alisema.

"Ankara itaendelea kuweka shinikizo kwa Israeli kupitia biashara, diplomasia hadi utawala wa Netanyahu utakapsitisha mauaji yake huko Gaza," alisisitiza.

Siku ya Ijumaa, ICJ ilithibitisha tena maagizo yake ya awali na kutaka kivuko cha Rafah kufunguliwa na kuruhusu wachunguzi kuingia kwenye eneo lililozingirwa.

Zaidi ya Wapalestina 35,900 wameuawa huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na karibu wengine 80,300 wamejeruhiwa tangu Oktoba kufuatia shambulio la Hamas.

Zaidi ya miezi saba ya vita vya Israel, maeneo makubwa ya Gaza yamegeuzwa magofu huku kukiwa na kizuizi cha chakula, maji safi na dawa.

Ukuaji wa asilimia 4.5

Rais pia aligusia malengo na mafanikio ya kiuchumi ya nchi.

Katika mafanikio ya kihistoria kwa Uturuki, mauzo ya nje yamezidi $255B, na kufikia rekodi ya $257.6B hadi Aprili, alisema.

"Ikiwa na kiwango cha ukuaji wa asilimia 4.5, Uturuki inashika nafasi ya kwanza barani Ulaya, ya pili katika nchi za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), na ya nne katika G-20," alisisitiza.

Akiashiria malengo ya mpango wa kiuchumi wa Ankara, rais wa Uturuki alisema, kwamba kipaumbele cha kiuchumi cha Uturuki ni kupunguza mfumuko wa bei hadi tarakimu moja kwa unafuu wa kudumu, huku tukizingatia utulivu wa muda mrefu ili kuboresha ustawi wa taifa.

TRT World