Usafi wa Mombasa: Tatizo la Taka Lapata Suluhu

Usafi wa Mombasa: Tatizo la Taka Lapata Suluhu

Mombasa yajinasua kutoka kwenye taka sugu. Udhibiti wa taka, ambao sasa umekabidhiwa kwa serikali za kaunti, umekuwa changamoto kwa taifa la Kenya kwa miaka mingi. Kaunti nyingi, ikiwa ni pamoja na Nairobi na Mombasa, zimetatizika kwa kiasi kikubwa kutokana na utupaji haramu wa taka na idadi ya watu inayoongezeka. Jiji la bandari la Mombasa linategemea tu jaa la taka ambapo taka nyingi takriban asilimia 90, hutupwa waziwazi au kuchomwa moto.