Jamaica imejiuna na nchi ambazo zinatambua Palestina kama nchi huru. / Picha: Getty

Jamaica imetangaza uamuzi wake wa kulitambua taifa la Palestina, ikiungana na nchi 141 wanachama wa Umoja wa Mataifa zinazotambua mamlaka ya Palestina.

"Jamaica inaendelea kutetea suluhu ya mataifa mawili kama chaguo pekee linalofaa kutatua mzozo huo wa muda mrefu, kuthamini usalama wa Israeli na kudumisha utu na haki za Wapalestina," Kamina Johnson Smith, Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Nje wa Jamaika, alisema katika taarifa siku ya Jumanne.

"Kwa kutambua Nchi ya Palestina, Jamaica inaimarisha utetezi wake kuelekea suluhisho la amani."

Majed Bamya, Naibu Mwangalizi Mkuu wa Nchi ya Palestina katika Umoja wa Mataifa, ameishukuru nchi ya Jamaica kwa uamuzi huo kupitia mtandao wa "X".

"Asante kwa kusimama upande wa amani, na haki ya watu wetu kujitawala," Amal Jadou, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina, aliandika kwenye mtandao wa X.

Kanuni zilizowekwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa

Waziri Smith alihusisha uamuzi wa Jamaica na wasiwasi mkubwa wa taifa hilo kuhusu vita vya Israel dhidi ya Gaza na mzozo wa kibinadamu unaozidi kuongezeka.

Badala ya kugeukia hatua za kijeshi, alisema, serikali inatetea mbinu ya kidiplomasia ya utatuzi wa amani kwa mzozo wa Israel na Palestina.

Uamuzi huu, kwa mujibu wa waziri, unaangazia kujitolea kwa Jamaica kwa kanuni zilizowekwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kukuza kuheshimiana na kuishi kwa amani miongoni mwa mataifa, huku ikitetea vikali haki ya watu kujitawala.

Smith pia alisisitiza uungwaji mkono usioyumba wa Jamaika wa kusitisha mapigano mara moja, kuongezwa kwa upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi walioathirika wa Gaza na uhuru wa mateka wa Israel.

Alisisitiza kushikamana na wanawake na watoto wengi wa Gaza ambao wamebeba mzigo mkubwa wa mateso ya kila siku, akisisitiza kujitolea kwa Jamaika kupunguza shida zao na kuwapa matumaini ya siku nzuri zijazo.

Jamaica imejitolea kwa suluhisho za kidiplomasia

"Jamaica inaendelea kuunga mkono juhudi zote za kupunguza vita kasi na uanzishaji wa amani ya kudumu katika eneo hilo, ikizitaka pande zote kuzingatia matokeo mabaya ya mzozo na kujitolea kwa suluhisho la kidiplomasia kuhakikisha usalama na uhuru wa wote," Smith aliweka wazi.

Uamuzi huo unakuja baada yanchi ya Barbados kutangaza uamuzi wake wa kuitambua rasmi Palestina kama nchi, na kuwa mwanachama wa 11 wa Jumuiya ya Karibea [CARICOM] kufanya hivyo.

"Tunawezaje kusema tunataka suluhu ya mataifa mawili ikiwa hatutambui Palestina kama Taifa," Waziri wa Mambo ya Nje wa Barbados Kerrie Symmonds alisema katika taarifa yake wiki jana.

TRT World