Al-aqsa mosque / Photo: AA

Wanajeshi wa Israel wamevamia eneo la Msikiti wa Al Aqsa na kuwashambulia waumini wa Kipalestina waliokuwa ndani, saa chache baada ya kuvamia eneo la tatu kwa Uislamu, jambo ambalo lilizua ukosoaji wa kimataifa.

Machafuko hayakuwa makali kuzidi shambulizi lililofanyika siku moja kabla. Lakini hali iliendelea kuwa tete kwani ni kipindi ambacho Waislamu waliadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani na Wayahudi walianza likizo ya wiki ya Pasaka.

Jeshi la Israel limesema roketi saba zilizorushwa kutoka Gaza mapema Alhamisi, zote zililipuka angani. Hakuna kundi lililodai kuhusika na hakuna majeruhi aliyeripotiwa.

Walioshuhudia wameliambia Shirika la Anadolu kwamba wanajeshi wa Israel walivamia Jumba la Swala la Al Qibli katika jengo la Msikiti wa Al Aqsa baada ya sala ya tarawih, sala maalum ya Waislamu wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani, wakarusha guruneti na kuwapiga waumini wa Kipalestina.

Wapalestina zaidi walikuwa wamekusanyika katika msikiti huo, wakiitikia wito wa kuswali ndani ya usiku kucha.

Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Palestina huko Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu ilisema timu zake za madaktari ziliwatibu Wapalestina sita, wawili kati yao wamelazwa hospitalini.

https://www.trtworld.com/middle-east/israel-troops-storm-al-aqsa-mosque-for-second-night-targeting-palestinians-66819

TRT World