Mwanamke wa Kipalestina akiwa ameshika mwili wa mtoto mdogo aliyeuwawa katika mfululizo wa mashambulizi hayo, Mei 26, 2024. / Picha: AFP  

Wapalestina 11 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mashambulizi manne ya Israeli katika eneo la makazi la Rafah, kusini mwa Gaza.

Duru za afya zimeliambia shirika la habari la Anadolu kuwa wapalestina sita waliuwawa na wengine kujeruhiwa baada ya nyumba yao kushambuliwa na bomu karibu na eneo la shule ya Al-Aqqad, kaskazini mwa Rafah.

Katikati mwa Rafah, majeshi ya Israeli yalilenga Wapalestina waliokuwa wamekusanyika katika eneo la mzunguko la Najma, na kuua watu watatu, vimeongeza vyanzo hivyo.

Jeshi la Israeli pia lilitumia kombora kumlenga Mpalestina kwenye mtaa wa Awni Dhair katikati mwa Rafah, pamoja na Mpalestina mwingine katika eneo la Khirbet Al-Adas upande wa kaskazini, kulingana na vyanzo hivyo.

Siku ya Ijumaa, ICJ iliiamuru Israeli kusitisha mashambulizi yake ya kijeshi katika eneo la Rafah, kufungua eneo la kuvukia ili kuruhusu upatikanaji wa taarifa muhimu.

TRT Afrika