| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Jimbo la Nigeria la Plateau lathibitisha kuwepo kwa maambukizi 11,000 ya Kifua Kikuu 2026
Maafisa wanaonya kuhusu kunyanyapaa na taarifa za kupotosha zinakwamisha baadhi ya wakazi kupata matibabu kwa wakati unaofaa.
Jimbo la Nigeria la Plateau lathibitisha kuwepo kwa maambukizi 11,000 ya Kifua Kikuu 2026
Nigeria bado ni moja ya nchi zenye maambukizi mengi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu duniani.

Jimbo la kaskazini katikati mwa Nigeria la Plateau limethibitisha karibu maambukizi 11,000 ya Kifua Kikuu mwaka 2026, huku wagonjwa 2,047 wakitambuliwa na kutibiwa kati ya mwezi Julai na Septemba, afisa mmoja wa afya amesema.

Yohanna Bot, afisa wa kutathmini maambukizi ya Kifua Kikuu katika jimbo hilo, aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano mji mkuu wa jimbo, Jos Jumapili jioni.

Bot, katika taarifa kwa Anadolu, alisema kuwa ugonjwa huo uliokadiriwa kuwa na maambukizi 219 kwa watu 100,000. Aliongeza kuwa wagonjwa waliotambuliwa wanaendelea kutibiwa katika vituo mbalimbali vya afya kwenye jimbo hilo.

Taarifa za kupotosha kuhusu Kifua Kikuu

Afisa huyo alionya kuwa unyanyapaa na taarifa za kupotosha kuhusu ugonjwa huo zinafanya baadhi ya wakazi kushindwa kutafuta matibabu.

Baadhi ya watu, anasema, bado wananasibisha ugonjwa wa Kifua Kikuu na sababu za kiimani pamoja na matambiko.

Ukosefu wa usalama na watu kuondolewa kwenye makazi yao kunakwamisha juhudi za kutambua na kutibu maambukizi, hasa eneo la Mangu, Jos Kusini na Barkin Ladi, ambapo vurugu zimesababisha wakazi kukimbilia kwenye makambi.

Nigeria bado ni moja ya nchi zenye maambukizi mengi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu duniani.

Ugonjwa huu unaweza kukingwa na kutibiwa, lakini kuchelewa kuutambua, kutofikia matibabu na kunyanyapaa kunaendelea kuwa changamoto katika kukabiliana na maambukizi.

CHANZO:َAA
Soma zaidi
Sisi wa Misri atafuta uungwaji mkono wa bunge ili kusaidia kuitetea Saudi Arabia kijeshi
Maambukizi ya Ebola nchini Kenya yapanda hadi saba kufuatia maambukizi mapya manne
Macky Sall wa Senegal ajiondoa katika kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Rais wa Misri asema ataondoka madarakani mwaka 2030, aahidi kutobadilisha katiba
Wagombea wote 7 wa nafasi ya Katibu Mkuu wa UN wanakabiliwa na kura ya turufu
DRC yasema rais wa zamani Joseph Kabila 'anapanga shambulio' baada ya kuungana na waasi wa M23
Kenya yathibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola- jamaa mwingine wa aliyekuwa na maambukizi ya kwanza
Nchi za Afrika zajiandaa kwa El Nino
Waziri Mkuu wa Ethiopia ateua serikali mpya ya Tigray, ataka uchaguzi ndani ya miezi sita
Tanzania kuondoa hatua za muda za usafiri wa anga
Mkuu wa polisi Afrika Kusini ruhsa kurudi kazini baada ya kufutiwa kesi ya ufisadi
DRC yakosoa uamuzi wa Formula 1 kuipa Rwanda uenyeji wa mbio za 'Grand Prix'
Kenya yalaani mashambulizi ya Wahouthi dhidi ya Saudi Arabia
Eritrea yakataa raia wake kurejeshwa kwa lazima kutoka Uingereza
Magaidi wa Boko Haram wawaua wanajeshi 10 katika shambulio la kambi ya jeshi nchini Nigeria
Algeria kuanza kutekeleza hukumu ya kifo kwa wanaochoma misitu, watekaji nyara watoto
Mvua kubwa yasababisha mafuriko ya ghafla Istanbul
Kenya yapandisha bei ya mafuta kufuatia mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati
Marekani yazitaka Ethiopia na Eritrea kupunguza mvutano
Kenya yathibitisha mgonjwa wa pili wa Ebola, ni jamaa yake wa kwanza aliyekuwa na maambukizi