Yusuf Kiranda, katibu wa chuo kikuu cha Makerere aliambia wabunge kupunguza bajeti ya chuo hicho kutaathiri mahitaji ya wnafunzi/Picha kutoka  Parliament Watch

Chuo kikuu cha serikali cha Makerere nchini Uganda kimepinga uamuzi wa serikali ya nchi hiyo kupunguza bajeti yake katika mwaka mpya wa fedha.

Uganda ina vyuo tisa vya umma vyenye kupokea bajeti kutoka kwa serikali huku vingine 44 vikiwa ni vya binafsi.

Serikali ya nch hiyo imependekeza kupunguza kiwango cha dola 6,867,540 ( shilingi bilioni 25.9) katika mwaka wa fedha wa 2024/25.

Uongozi wa chuo hicho unasisitiza kuwa maamuzi hayo yataathiri ubora wa huduma zitolewazwo na taasisi hiyo ya elimu.

Yusuf Kiranda, Katibu wa Chuo Kikuu cha Makerere aliwaambia wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa uamuzi huo utasababisha wanafunzi kukosa vitu vingi kwa muhimu.

"Sijaona Chuo Kikuu kingine chochote cha umma ambacho kilichowahi kutekeleza mpangilio huu mekumbwa na kupunguzwa kwa bajeti kama Chuo Kikuu cha Makerere, " Kiranda ameambia kamati hiyo ya bunge.

Mwaka 2023/24 Chuo Kikuu cha Makerere kilitengewa dola 98.687,351 (Shilngi bilioni 372.186) lakini, bajeti ya Chuo hicho inatarajiwa kushuka hadi dola 93,862,572 (Shilingi bilioni 353.99) kwa mwaka 2024/25

Katika bajeti hii mpya mishahara itagharimu dola 5,5409,649 (Shilingi bilioni 208.970), huku mahitaji mengine yakipewa dola 34,375,354 (shilingi bilioni 129.642), wakati bajeti ya Maendeleo imetengewa 4.075.978 (Shilingi bilioni15.372)

TRT Afrika