Makubaliano Ethiopia

By Coletta Wanjohi

Mamlaka ya maendeleo ya kiserikali, IGAD, inasema uamuzi wa Ethiopia kwakuondoa kikundi cha Tigray People's Liberation Front, TPLF, kutoka kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi itaongeza imani katika utekelezaji wa mchakato wa amani kaskazini mwa nchi.

“Hii itaipa nguvu mkataba wa kudumu wa kukomesha uhasama uliotiwa saini Novemba 2022 mjini Pretoria,” anasema Workneh Gebeyehu, katibu mtendaji wa IGAD, “hatua hiyo itaimarisha imani kati ya pande hizo.”

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ilitia saini mkataba wa amani na kundi hilo la TPLF, tarehe 2 Novemba 2022, ili kumaliza mzozo ulioanza Novemba 2020.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 9.7 katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo wameathiriwa na ugomvi huo.

Bunge ya Ethiopia ambayo iliitaja kundi hilo kama kundi la kigaidi mnamo Mei 2021, imesema imeamua kugeuza uamuzi huo, "ulikuwa muhimu kwa utekelezaji wa makubaliano ya amani".

Tunajua nini kuhusu kundi la Tigray People’s Liberation Front, TPLF?

-TPLF ilianza mwaka wa 1975 kama kikundi kidogo cha waasi

- Kuanzia 1989 hadi 2018 iliongoza muungano wa kisiasa wa mapinduzi uitwao Ethiopia Revolutionary Democratic Front

-Iliongoza vita dhidi ya serikali ya Derg iliyotawala nchi hiyo kwa miaka 17 chini ya Meja Mengistu Haile Mariam. Sheria hiyo ilipinduliwa mnamo 1991

- TPLF iliunda serikali mpya nchini Ethiopia mwaka 1991 na kubakia madarakani

-TPLF iliondolewa kutoka kwa udhibiti wa serikali ya shirikisho mnamo 2018 baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kuchukua madaraka

- Tarehe 3 Novemba 2020 mzozo ulitokea kati ya serikali ya Ethiopia na TPLF

- Mnamo 2021, bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya Ethiopia ilighairi usajili wa kisiasa wa TPLF ikiishutumu kujihusisha na vita.

- Tarehe 6 Mei 2021 Bunge la Ethiopia liliorodhesha TPLF kama kundi la kigaidi

-Tarehe 2 Novemba 2022 Serikali ya Shirikisho la Ethiopia na TPLF zilitia saini makubaliano ya amani makubaliano huko Pretoria Afrika Kusini kumaliza mzozo wa miaka miwili Kaskazini mwa Ethiopia

TRT Afrika