TikTok Oracle / Photo: AP

Mtendaji Mkuu wa TikTok amekabiliwa na maswali magumu kutoka kwa wabunge ambao wanaamini kuwa mtandao wa TikTok inaomilikiwa na Uchina unapaswa kuzuiwa kwa kuwa "chombo" cha Chama cha Kikomunisti cha China na kwa sababu una maudhui yanayoweza kudhuru afya ya akili ya watoto.

Wanachama wa Republican na Democrats pia waliibua wasiwasi mwingi kuhusu uwezekano wake wa kutishia usalama wa taifa la Marekani kwa kugawa data zake na serikali ya China.

Alipoulizwa ikiwa wamiliki wake wa Uchina wata acha kuwekeza Marekani, Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok Shou Zi Chew alijibu, "sio juu ya umiliki," na kuongeza, "Mitandao ya kijamii ya marekani haina rekodi nzuri ya faragha za taarifa binafsi na usalama wa watumiaji. Namaanisha, angalia Facebook na Cambridge Analytica."

TikTok imesema imetumia zaidi ya dola bilioni 1.5 kwa kile inachokiita juhudi kali za usalama wa taarifa binafsi chini ya jina "Project Texas" ambayo kwa sasa ina karibu wafanyakazi 1,500 na ina mkataba chini ya Oracle Corp ORCL.N kuhifadhi data ya watumiaji wa TikTok marekani.

Kampuni hiyo pia inasema inakagua kwa uangalifu maudhui ambayo yanaweza kuwadhuru watoto.

Reuters