Rwanda imekewekeza vikubwa katika utalii wa mikutano / Picha: AA

Rwanda imekewekeza sana katika utalii wa mikutano. Hii inahusiha kuvutia mikutano ya kimataifa ya aina tofauti mwaka mzima.

Na hii inaonekana kufua dau mwaka baada ya mwingine. Ofisi ya Mikutano ya Rwanda inasema Sekta ya Mikutano, Motisha, Mikutano na Matukio ya Rwanda (MICE) ilirekodi mapato ya dola milioni 95 mwaka 2023.

Hii ni ongezeko kutoka 2022 ambapo nchi hiyo ilizalisha dola milioni 64 katika mapato ya mikutano.

Mapato hayo yalitokana na jumla ya mikutano 160 ambayo Rwanda iliandaa, ambayo yalivutia zaidi ya watu 65,000 mwaka 2023.

Kulingana na takwimu za nchi hii ni mapato ya juu zaidi yaliyopatikana katika muongo mmoja uliopita .

"Pamoja na wahusika wengine wa tasnia, tumeonyesha uthabiti na kubadilika, na kusisitiza dhamira yetu ya kuunda thamani na kudumisha ukuaji wa muda mrefu," alisema," Fred Swaniker, Mwenyekiti wa Bodi ya RCB amesema.

Utalii wa michezo uliimarika mwaka 2023 wakati Rwanda ilipopata ongezeko kubwa la idadi ya hafla za michezo, na washiriki 13,785 walivutiwa katika hafla 27, na kuashiria ongezeko kubwa la asilimia 59 ikilinganishwa na hafla 17 mnamo 2022.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, zaidi ya mikutano 90 yamethibitishwa kuandaliwa nchini Rwanda mwaka 2024.

Kati ya hizi, RCB inapanga kuandaa hafla 45 ili kupata mapato ya $32 milioni kwa miaka ijayo.

TRT Afrika