Kikundi cha wanajeshi Niger wametangaza kuwa serikali imepinduliwa / Photo: Reuters

Wanajeshi wa Niger wamesoma taarifa kwenye televisheni ya taifa wakisema Rais Mohamed Bazoum ameondolewa madarakani.

Wanajeshi hao waliongeza katika tangazo hilo Jumatano usiku kwamba maeneo yote ya mpaka wa Niger yamefungwa kwa muda usiojulikana, na kwamba taifa litakuwa chini ya amri ya kutotoka nje usiku kila siku.

"Sisi, vikosi vya ulinzi na usalama tumeamua kusimamisha utawala wa Rais Bazoum," Luteni Kanali Amadou Abdramane alisema.

Wakati wa hotuba yake, alizungukwa na askari wengine tisa waliovaa sare. Wanajeshi hao waasi walisema "taasisi zote" nchini zitasitishwa.

Kauli hiyo inajiri baada ya walinzi hao wa rais mapema Jumatano kumweka mkuu wa nchi katika ikulu ya rais katika mji mkuu Niamey.

Kilichosababisha mapinduzi hayo hakijulikani kwa sasa. Niger imekuwa ikipambana na uasi wa kudumu ambao umesababisha vifo vya raia wengi, wanajeshi na maafisa wengine wa usalama.

Mpito wa kwanza kabisa wa mamlaka ya kidemokrasia nchini Niger ulifanyika Aprili 2, 2021, wakati Bazoum alipopokea vyombo vya mamlaka kutoka kwa mtangulizi wake, Mahamadou Issoufou, ambaye alijiuzulu kwa hiari.

ECOWAS na Umoja wa Afrika zakashifu mapinduzi ya serikali

Jumuiya ya uchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, ECOWAS, imekashifu mapinduzi ya serilai Niger na kuwataka wanmajeshoi hao kumuachilia rais na familia yake na wajumbe wengine huru, bila masharti.

Mwenyekiti wa ECOWAS ambaye pia ni rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ametangaza Jumatano jioni kwamba ECOWAS ilimtuma Rais wa Benin Patrice Talon kwenda Niger kusaidia katika kuzuia uwezekano wa mapinduzi.

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Mahammat Faki pia amekashifu kitendo hicho alkiwaita wanajeshi hao wahaini.

TRT Afrika