Ziara rasmi ya William Ruto imezua gumzo nchini Kenya. /Picha: Ikulu ya Kenya

Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa kukodi ndege binafsi kwa ajili ya safari yake ya Marekani wiki jana ni kwa sababu ya kupunguza gharama.

Ruto alikaribishwa na Rais Joe Biden mnamo Mei 23 katika ziara rasmi ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Afrika tangu 2008.

Ripoti nchini Kenya zilisema kuwa serikali ilitumia shilingi milioni 200 (dola milioni 1.5) kukodi ndege hiyo ya kibinafsi kutoka kwa kampuni ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

"Wakenya wenzangu, nimeona kuna wasiwasi kuhusu usafiri wangu hadi Marekani. Kama msimamizi anayewajibika wa rasilimali za umma na kwa kuzingatia azma yetu kuishi kulingana na uwezo wetu, na wajibu kuwa safu ya mbele kutoa mfano bora, gharama ya kusafri ilikuwa chini ukilinganisha na kusafiri kwa ndege ya Kenya Airways," Ruto alisema hivyo kupitia mtandao wa kijamii wa X, siku ya Jumapili.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na "Voice of America" , Ruto alisema gharama ya ndege ya kibinafsi ya dola milioni 1.5 "ilichochewa" na ya "kuchekesha."

TRT Afrika